• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 8:55 AM
Msanii kutoka Tanzania akana kuzaa Kenya 

Msanii kutoka Tanzania akana kuzaa Kenya 

NA RAJAB ZAWADI
WIKENDI iliyotuacha, staa wa bongo flava Mbosso Khan alitua Mombasa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye dimba la dondo la mtangazaji wa runinga Rashid Abdalla Cup.

Wakati anatua, kuna msanii chipukizi kwa jina Demah B ambaye amekuwa akidai kuwa nyota huyo wa lebo ya WCB Wasafi, ni babake mzazi.

Wapo walioamini kutokana na kuwepo na kiwango fulani cha wawili hao kufanana.

Lakini kwa kuwa ni madai, ambayo yalimhusu Mbosso ilikuwa ni sahihi yeye kuyaweka sawa.

Na kwenye kunyoosha mambo, Mbosso alijigeuza mbogo na kukana kuwa babake msanii huyo Mkenya.

“Yule namwona kupitia mitandao ya kijamii sasa tatizo sio tatizo. Kutokana na umri wake, kutokana na yeye mwenyewe alivyo, ananitia uwoga hadi mimi nahisi pengine yeye ndiye babangu. Unajua yeye mwenyewe anaonekana mkubwa hadi kanizidi mimi. Kwa hiyo kama yeye anaona mimi ni babake, na mimi nahisi kama yeye ndiye babangu. Sasa sijui itakuwaje hapo,” Mbosso  kakata kauli.
Demah B aliibuka kutokea machimbo yake na kudai kuwa Mbosso kama babake kamtelekeza.

Msanii huyo alidai kuwa yeye wakati akiwa anateseka huku Kenya akiishi maisha ya uchochole, babake Mbosso yupo vizuri kule Tanzania akila bata kweli kweli.

“Huyo jamaa (Mbosso) tuseme tu ni kama amekataa majukumu anaogopa DNA. Kwangu mimi niko tayari kufanya DNA tujue kama mimi ni mtoto wake, sababu ameniacha nateseka hapa Kenya na babangu yuko kule majuu. Mimi nataka kumwambia Mbosso tufanye DNA tujue ukweli uko wapi,” Demah B alidai.

Msanii Mbosso Khan ambaye majina yake halisi ni Mbwana Yusuph Kilungi, alizaliwa Oktoba 3, 1995 Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, na mcheza ala za muziki chini ya lebo yake; WCB Wasafi, ambayo ni kati ya tajika zaidi Afrika Mashariki.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Mlinzi auawa katika uvamizi wa Kanisa la PCEA Rironi, wezi...

Waititu: Nilipotoshwa na uongozi wa UDA

T L