• Nairobi
  • Last Updated April 12th, 2024 4:55 PM
Waititu: Nilipotoshwa na uongozi wa UDA

Waititu: Nilipotoshwa na uongozi wa UDA

NA WANDERI KAMAU

ALIYEKUWA gavana wa Kiambu, Bw Ferdinard Waititu BabaYao, amesema kuwa ashahama na kujiondoa katika chama cha United Democratic Alliance (UDA) ambacho ndicho kikubwa katika serikali ya Kenya Kwanza, akidai kwamba alipotoshwa.

Bw Waititu alikitaja chama hicho kama kilichojaa viongozi wadanganyifu.

“Nilipotoshwa. Nilikuwa na matumaini mengi nilipojiunga na UDA, japo nilibaini kuwa viongozi wengi katika chama hicho ni wanafiki,” akasema Bw Waititu, Jumanne, kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio.

Bw Waititu pia alisema kuwa ahadi zote ambazo alipewa, ikiwemo kupewa kazi serikalini zilikuwa hewa tu.

Mnamo Desemba 2022, Rais Ruto alimteua Bw Waititu kuwa mwanachama katika Tume ya Mto wa Nairobi (NRC), lakini uteuzi wake ukafutiliwa mbali na mahakama, kutokana na kesi ya ufisadi ambayo imekuwa ikiendelea dhidi yake.

Kwenye uchaguzi wa Agosti 9, 2022, Bw Waititu alijiunga na mrengo wa Kenya Kwanza na kutangaza kumuunga Rais William Ruto (wakati huo akiwa Naibu Rais) kuwania urais.

“Wale walionipa kazi walikuwa washapanga kuhusu vile ningenyang’anywa. Hivyo, kupewa hiyo kazi kunafanana na mbwa aliyerushiwa mfupa na baadaye akanyang’anywa,” akasema Bw Waititu.

Wakati huo huo, gavana huyo wa zamani aliwalaumu wanasiasa kutoka ukanda wa Mlima Kenya kwa kutowatetea wenyeji vilivyo, kutokana na changamoto zinazowaathiri.

Alisema wengi wao wamekuwa wakinyamazia changamoto zinazowakumba wenyeji, kwa kuhofia kuonekana kuwa ‘waasi’ dhidi ya serikali.

  • Tags

You can share this post!

Msanii kutoka Tanzania akana kuzaa Kenya 

UDAKU: Harmonize adai amekosa kolabo na Davido kwa sababu...

T L