• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:50 AM
MUME KIGONGO: Kunywa kahawa kunasaidia wanaume wenye kansa ya tezi dume

MUME KIGONGO: Kunywa kahawa kunasaidia wanaume wenye kansa ya tezi dume

NA CECIL ODONGO

KUNYWA kahawa kwa wingi kunasaidia wanaume ambao wanaugua kansa ya tezi dume (prostate cancer) kuishi muda mrefu, watalaamu wamebaini.

Utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Texas Amerika unaonyesha kuwa wanaume wana jeni spesheli ambayo ikipatana na kafeni iliyoko ndani ya kahawa, huibuka na kemikali ambayo huua seli za kansa ya tezi dume.

Dkt Justin Gregg wa chuo hicho, ambaye ni kati ya wataalamu waliofanya utafiti huo, alisema kuwa kemikali inayofahamika kisayansi kama CYP1A2 AA ina miale kali ambayo hupunguza makali ya kansa katika kiwango chochote kile mwilini.

“Huu ni utafiti ambao utastahili kuzamiwa zaidi kwa sababu kuna maswali mengi kuhusu jinsi vyakula vinavyoliwa huchangia kansa ya tezi dume. Hata hivyo, tulibaini kuwa wanaume ambao hunywa kahawa kwa wingi hawakulemewa na kansa ya tezi dume kama wale ambao hawakuinywa kahawa,” akasema Mtaalamu Gregg.

Pia kafeini kwenye kahawa huondoa uchafu katika tezi dume na kupunguza kasi ya viini vya kansa kuenea mwilini. Wanaume hasa huwa katika hatari ya kupata saratani kutokana na mtindo wao wa maisha wa kubugia pombe na uvutaji wa sigara.

Kulingana na takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyochapishwa mnamo 2020, kansa ya tezi dume huchangia asilimia 0.49 ya vifo vyote nchini na Kenya iliorodheshwa 51 duniani kati ya nchi ambazo kansa hiyo husababisha vifo vingi.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Teknolojia ya ‘3D printing’ yaleta...

Wanjigi asema waliopoteza uchaguzini wasiteuliwe makatibu...

T L