• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 7:50 AM
NASAHA ZA RAMADHAN: Itambue siri kubwa ya ibada ya kufunga Ramadhani

NASAHA ZA RAMADHAN: Itambue siri kubwa ya ibada ya kufunga Ramadhani

Na ATHMAN FARSI

MWENYEZI Mungu anawapenda wale wanaofunga kwa kutimiza masharti yote, na ameahidi ujira mwema kwa wanaofunga.

Kufunga ni kujiepusha na kula, kunywa, kujiepusha kufanya mabaya na mengineo.

Katika huu mwezi waumini wa Kiislamu hufunga kila siku kwa muda wa siku ishirini na tisa au thelathini (kulingana na mwandamo wa mwezi wa shawwal) kutoka alfajiri hadi machweo wakati ambao saumu huvunjwa na kuanza kula tena hadi siku ifwatayo.

Kwa mukhtasari tu, Saumu ya Ramadhani imefaradhishwa na ni wajibu kwa kila muumini muisilamu wa kiume na wa kike ili kumkurubia Mwenyezi Mungu.

Halikadhalika kufunga huwezesha muumini kujitambuwa, kujizuia na matamanio, kukumbusha siku ya kiama na hivyo basi kujizatiti kutenda mema na kujianda kuwa mtu mwema kwa kufuata njia ilionyooka ya kujikita na mema peke yake maishani.

Lakini ni nini siri na athari ya kufunga saumu ya Ramadhani?

Mojawapo ya athari ya kufunga kwa mwenye kufunga ni kuwa inakatiza mazoea ya tabia, matamanio na humuweka mtu huru na hisia za kimwili. Mtu aliye huru ni yule ambaye licha ya uraibu ama tabia fulani huuthibiti kwa kujizuia ule uraibu bila shida yeyote.

Uhuru wa aina hii humpelekea mfungaji kupiga hatua inayomuwezesha kufinikia malengo ya kufunga.

Kufunga saumu ya Ramadhani huhusisha hisia za kiimani. Kitendo cha kufunga humfanya mfungaji kukumbuka njaa ya mafakiri na masikini na humuwezesha kutambuwa uwepo wa shida na mateso maskini hupitia.

Mfungaji akifikia hii daraja ya kuwahurumia mafakiri basi natija yake ni kuondoa daraja mbali mbali za watu na kufanya mfungaji kutekeleza zoezi la kuwasaidia wasiojimudu kimaisha.

Kufunga huleta umoja kwasababu waumini masikini na matajiri wote wanapitia hali sawa nyakati za kufunga nazo ni hali za kujitenga na matamanio mbali mbali.

You can share this post!

IRENE MUKUSYA: Ninalenga kupaa anga za kimataifa kwa...

Korti yatupa baadhi ya ushahidi wa mume anayetaka kutaliki...