• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Hii hapa siri ya kujipatia ngozi ya kupendeza

Hii hapa siri ya kujipatia ngozi ya kupendeza

· Lishe: Bila shaka uhai wa ngozi unategemea na unachokula. Vyakula vilivyo na viwango vya juu vya sukari na mafuta huharakisha ngozi kuzeeka. Kwa upande mwingine vyakula vilivyo na viwango vya juu vya nyuzi kama vile mboga na matunda ni muhimu kuhakikisha kuwa ngozi yako inakuwa thabiti kwa muda mrefu.

· Jua: Bila shaka jua ndio chanzo cha vitamini D, virutubisho muhimu kwa ngozi. Lakini kujiweka wazi kwa miale yake kwa muda mrefu pia kuna madhara yake. Mbali na kukuweka kwenye hatari ya kukumbwa na kansa ya ngozi, miale mikali ya jua, hufanya ngozi kuwa nyepesi na kuzeeka upesi. Kadhalika unashauriwa usijiweke wazi kwa jua kati ya saa nne asubuhi na saa tisa alasiri kwa sababu wakati huu miale huwa na nguvu sana.

· Mafuta: Kila unapoenda kwa jua hakikisha kuwa unajipaka mafuta ya sun screen. Kadhalika unapochagua mafuta haya hakikisha kuwa yana kiwango cha kulinda dhidi ya miale- sun protection factor (SPF) cha 15 au zaidi. Kadhalika mikono na uso huwa wazi sana kwa jua kwa hvyo ifunike unapotembea kwa jua.

· Vitu muhimu: Hivi ni vifaa ambavyo vitakusaidia kupunguza uwezekano wa ngozi kuzeeka hasa unapotembea kwenye jua. Baadhi ya vitu hivi ni pamoja na:

· Kofia: Valia kofia yenye ukingo. Hii huzuia miale ya jua isifikie tu macho pia ngozi inayozunguka sehemu hii ambayo kwa kawaida huwa nyepesi.

·Miwani: Husaidia kukinga macho na ngozi inayozunguka sehemu hii kutokana na miyale mikali ya jua.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi uharibifu wa Milima ya Shella unavyohatarisha Lamu...

Madiwani wa UDA Nairobi wapanga njama kung’oa kiongozi wa...

T L