• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 2:24 PM
Infinix yazindua simu mpya aina ya NOTE 30 series

Infinix yazindua simu mpya aina ya NOTE 30 series

NA WINNIE ONYANDO

KAMPUNI ya kutengeneza simu ya Infinix imezindua aina mpya ya simu iliyo na uwezo wa kunasa picha bora.

Simu hiyo aina ya NOTE 30 inajumuisha NOTE 30 Pro, NOTE 30 VIP, na NOTE 30.

Kadhalika, simu hiyo mpya inajivunia skrini yenye kiwango bora cha 120Hz na kamera tatu ulio wazi sana na lensi yenye hadi 108MP.

“Simu yenyewe ina skrini ya hali ya juu, kamera nzuri sana, mfumo wa sauti uliopangwa vizuri na uwezo wa kuiunganisha jamii. Bila shaka simu hii ni chaguo bora kwa watumiaji wote,” Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Infinix Liang Zhang akasema.

Naye Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye alikuwa mgeni mkuu mwalikwa katika uzinduzi huo aliwahimiza vijana nchini kujiajiri kupitia nafasi zinazopatikana mitandaoni.

“Kuna simu kadhaa ambazo bei zao ni nafuu. Ikiwa vijana watanunua simu kama hizo na kutengeneza video basi wataweza kujikimu kimaisha,” akasema Gavana Timamy wakati wa uzinduzi wa simu mpya aina ya NOTE 30 Series.

Kadhalika, alidokeza kuwa kuna wasanii wengi ambao wamejiajiri kupitia njia kama hiyo.

Simu aina NOTE 30 Series iliyozinduliwa ni ya ubora wa hali ya juu. PICHA | WINNIE ONYANDO

Simu hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Infinix inalenga wasanii wa kutengeneza video za mtandaoni.

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika siku chache tu baada ya Rais William Ruto kuwahimiza vijana kukumbatia mitandao ya kijamii kama vile TikTok kujiajiri.

  • Tags

You can share this post!

Machifu maadui wa maendeleo wamulikwa Kilifi

Mradi wa Sh110 milioni wageuka makao ya panya

T L