• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Kanisa lafungisha ndoa za pamoja kusaidia kupunguza tabia za ukora wa kimapenzi Teso Kaskazini

Kanisa lafungisha ndoa za pamoja kusaidia kupunguza tabia za ukora wa kimapenzi Teso Kaskazini

KNA NA FRIDAH OKACHI

Wanandoa 49 walifunga pingu za maisha katika misa Kaunti ndogo ya Teso Kaskazini iliyofanyika kwenye Kanisa la Katoliki la Parokia ya Chelelemuk Nobemba 18, 2023.

Askofu wa Katoliki jimbo la Bungoma Mark Kadima aliongoza harusi hiyo iliyohudhuriwa na kasisi wa Parokia hiyo Bernard Famba.

Zaidi ya wanandoa 100 walikuwa wamepangwa kufunga ndoa, lakini ni 49 pekee walioweza kufika mbele ya Askofu Kadima ili kupewa sakramenti takatifu ya ndoa.

Furaha ilitanda huku wapenzi hao wakila kiapo kabla ya kuvishana pete za ndoa.

Bw Kadima alihubiri kuhusu upendo na heshima miongoni mwa wanandoa akisisitiza haja ya kuishi kwenye ndoa haramu badala ya mazoea ya wapenzi kuishi kinyumba.

Askofu alikiri kujawa na furaha kwa kuhudhuria harusi hiyo.

“Pendaneni na kuheshimiana. Mwenyezi Mungu atabariki ndoa zenu,” alisema Askofu huyo.

Harusi ya kwanza ya umati katika parokia hiyo ilifanywa mnamo Novemba 26, 2022 ambapo wanandoa 61 walifunga ndoa katika harusi ya kihistoria ya Teso Kaskazini.

Waandalizi wa sherehe hizo mbili walisema zilikusudiwa kuhakikisha wanandoa wengi katika Parokia hiyo wanapokea sakramenti ya ndoa kama ilivyoainishwa kwenye Biblia.

Askofu Kadima aliwapongeza wanandoa kwa kujitolea na kuwahakikishia kuungwa mkono na kanisa katika maisha yao ya ndoa.

Alisema ndoa ni onyesho la upendo kutoka kwa Mungu.

“Ni katika ndoa Mungu anaonyesha upendo wake. Kwa mwanamume na mwanamke kukubaliana kujitolea kupendana kwa maisha yao yote. Inamaana dhabihu zote zimetolewa. Ndoa si uamuzi wa mtu binafsi, ni uamuzi unaotoka kwa Mungu,” alisema.

“Ni mwito kutoka kwa Mungu kwa yule unayeoa. Mungu hupea kila mmoja. Hivyo, tunaomba wasalie kuwa uaminifu kwa wapenzi wao,” aliongezea.

Kasisi alisema wanandoa hao wanafaa kuwa tayari kutoa dhabihu kwa yule ambaye ndoa yake itafeli.

Askofu aliwataka wanandoa hao wapya kujitolea kwenye ndoa zao na maisha yao.

  • Tags

You can share this post!

El Nino yaangamiza watu 4 Wajir mafuriko yakilemea kaunti...

Viwanda vya chai vyabaki pweke Murang’a wakulima wakiuza...

T L