• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mke wa mwanasoka Ezekiel Otuoma adhihirisha mapenzi ya dhati kwa kumtunza kipindi chote akiugua

Mke wa mwanasoka Ezekiel Otuoma adhihirisha mapenzi ya dhati kwa kumtunza kipindi chote akiugua

NA FRIDAH OKACHI

MKE wa mwanasoka Ezekiel Otuoma, Racheal Otuoma ameapa kamwe hatamuacha bali ataendelea kumfaa kipindi chote kigumu anapokabiliana na ugonjwa. 

Bi Otuoma ambaye ni mpambaji mashuhuri, alisema mumewe alimuonyesha mapenzi ya kweli hivyo hawezi akamuacha wakati huu anapohangaika, licha ya marafiki wake kumshauri ajiondoe kwa ndoa hiyo.

Mchezaji Otuoma alichezea timu ya Stima na kuzidiwa na ugonjwa wa neurone unaojulikana kisayansi kama amyotrophic lateral sclerosis. Ugonjwa huo umemsababishia mchezaji huyo madhila  kukosa uwezo wa kumwezehdutembea mwenyewe, kuongea na hata kujilisha.

Mchezaji huyo alianzia taaluma yake kwenye timu Muhoroni mwaka mmoja baadaye alielekea Ulinzi, Western Coaches, AFC Leopards, SoNy Sugar, Ushuru na kisha Talanta ambapo alianza  kuugua mwaka 2019.

Kulingana na Bi Otuoma, mumewe alianza kupoteza sauti na kufikiria ni homa ya kawaida. Baada ya vipimo kadhaa katika Hospitali ya Kenyatta, waliambiwa ugonjwa huo ulikuwa umemuathiri kiakili na hata viungo vyake.

“Nilitoka India ndipo nikaanza kukubali ukweli huo,” alisema Bi Otuoma, akiongeza wataalam walimueleza hali hiyo ni ya kudhibiti tu.

Bi Otuoma aliapa hawezi kumwacha kutokana na maisha ambayo alimpea kipindi alikuwa akisakata boli na akiwa sawa kiafya.

“Kitambo tuliishi kwenye maisha ya umaskini, lakini tulijipata kwenye hali nzuri na siwezi toka,” alisema Bi Otuoma.

“Otuoma alinipea maisha, nilimjua kama hana chochote. Walikuwa wakiishi na mamake, nilimkubali na kunipeleka kwenye nyumba ya mabati na nikamkubai. Wakati alikuwa na pesa hakubandilika,” alisisitiza Bi Otuoma.

Mkewe Otuoma alisema kuna kipindi walikosa pesa na kuogopa kurudi kwa watu akihofia masimango.

Bi Otuoma alisema marafiki wengi walimpa mawaidha ya kuondoka kwenye ndoa yake, jambo ambalo alisema kuwa katu hawezi.

Jinsi muda unavyosonga, mkewe mchezaji huyo amesema wachezaji wenzake pamoja na marafiki wengine walianza kumtoroka.

  • Tags

You can share this post!

KCSE: Kinaya cha walimu wengi kumulikwa kwa udanganyifu...

Gaucho: Ni kinaya waliofanya maamuzi mabaya debeni wanataka...

T L