• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
PENZI LA KIJANJA: Urembo ni bonasi, gharimikia uhusiano

PENZI LA KIJANJA: Urembo ni bonasi, gharimikia uhusiano

NA BENSON MATHEKA

IKIWA unadai unapenda mwanamume ilhali kazi yako ni kutaka akutimizie na kukidhi mahitaji yako yote, utajua haujui.

Kizazi cha wanaume wa sasa kimechanuka na hakitaki wanawake wa mzigo na hasara kwao. Wanataka kutumia mali yao kwa wanawake wanaotumia yao kwao pia. Sio wanaozoea kuomba nauli, wanaitafuna na kuingia mitini.

Na hulka hii ya wanaume imesababishwa na vipusa wa kisasa ambao wataalamu wanasema wamepungukiwa na utu na kuchagua kuwa kupe wa kuwafyoza na kuwafilisisha.

“Wanaume wamekuwa wajanja zaidi kuliko vipusa. Wanakwepa wasioweza kujilipia nauli kutembelea mtu wanayedai wanapenda,” asema mwanasaikolojia Ruth Odili na kuongeza kuwa wanaume wanaambaa vipusa wakigundua wanawasababishia hasara.

“Mtu anayedai anapenda mwanamume atagharimika kumtembelea. Hatakuwa akiomba fare kila wakati kwenda kukutana naye kwa burudani kana kwamba yeye hafurahii wanachofanya faraghani,” asema Odili.

Kulingana na mwanasaikolojia huyu, tabia ya kula fare ya vipusa imewafanya wanaume kuwaogopa.

“Unapata kidosho hawezi kununulia mpenzi wake zawadi ya siku wa wapendanao au ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, ilhali anatarajia mpenzi wake amwandalie ya kukata na shoka kisha anakasirika na pengine kumtema akikosa kufanya hivyo,” asema Odili.

Kulingana na mwanasaikolojia Ivan Swaka, tabia nyingine inayofanya vipusa kuhepwa na wanaume wanaodai wanawapenda ni kutaka wawapigie simu.

“Unapata kazi ya mwanadada ni kuflash simu, kulalamika mwanamume ampigie simu na kuomba bundles na credo ya simu. Wanaume wamekuwa wakihepa wanawake wenye tabia kama hii ambao hawawezi kugharimika kwao,” asema Ivan.

Mwanasaikolojia huyo anasema vipusa wamekuwa wakijiletea balaa kwa kubadilisha uhusiano wa kimapenzi kuwa ajira ambapo anapaswa kulipwa na kutunzwa kwa kuwa wanawalisha uroda wanaume.

“Uroda haufaidi wanaume pekee. Kila mtu anafurahia kurushana roho na hivyo basi tabia ya akina dada kuamini ni lazima mwanamume agharamike kwao ili wamuonjeshe tunda ni unafiki,” asema na kuongeza kuwa mwanaume anachoshwa na kipusa anayekataa kumfungulia mzinga kwa kukosa kukidhi baadhi ya mahitaji yake mara moja hata kama amekuwa akitumia mamilioni kwake.

Kulingana na Odili, wanaume wanakatiza uhusiano wa kimapenzi na mwanamke hata kama amejaliwa umbo na urembo wa malkia.

“Urembo ni bonasi katika uhusiano wa kimapenzi, wanaume wanalenga na kuzingatia zaidi ulivyo kama mwanamke na kukwamilia kwa wale wanaoweza kuongeza kitu cha thamani katika maisha yao,” aeleza.

Mwanasaikolojia huyo anataja vitu ambavyo wanaume wanasaka kwa vipusa kama akili ya kutafuta pesa badala ya kuwafyoza, akili ya kudhibiti hisia na maisha yao ya kiroho.

“Haya ni mambo matatu ambayo mwanamke akiwa nayo, hakuna mwanamume mwenye akili timamu anaweza kutaka amuache,” aongeza.

  • Tags

You can share this post!

Patashika EPL Arsenal, Man-U wakisaka ubabe

BAHARI YA MAPENZI: Mdada pia ana haki ya kumrushia chali...

T L