• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 9:49 AM
SHANGAZI SIZARINA: Mbona kila ninayemtongoza anikataa?

SHANGAZI SIZARINA: Mbona kila ninayemtongoza anikataa?

Mbona kila ninayemtongoza anikataa?

Kusema ukweli nahisi kama nimelaaniwa, kwani kila ninapotongoza huwa nakataliwa. Nifanyeje kwani nimekata tamaa ya kuwa katika uhusiano.

M.H. Marereni

Inawezekana lugha unayotumia sio rafiki na ndio maana unakataliwa. Jaribu kubadilisha lugha na jinsi ambavyo unazungumza na hao wasichana.

Sina hisia za mapenzi, nina kasoro?

Mimi ni msichana wa umri wa miaka 19, wanaume wanipenda sana nami sijawahi sikia nimependezwa na hata mmoja wao. Pia sina hisia za kupenda. Hata mwanamume akinifuatilia, huwa namchukia na sitaki kumuona na ikibidi huwa namtoroka. Je, nina kasoro?

Sidhani kama una kasoro, isipokuwa unahitaji kukomaa zaidi na kuelewa zaidi masuala ya mapenzi. Huenda pia kukutana kwako na hao wanaume kumekuwa na changamoto na hujawahi kuona ama kutendewa yaliyo mema katika mapenzi.

Nimechoka na upweke, naomba unisaidie kupata mke

Shangazi mimi nina umri wa miaka 29 na najua huwa unasaidia sana watu. Nahitaji unisaidie nipate mke kwani nimechoka kuishi peke yangu.

James, Mpeketoni

Mbona mwenzio hiyo kazi ya ukuwadi wala hainihusu. Jitahidi uangalie jinsi utaweza kumpata.

Kwetu ajulikana lakini hataki kunipeleka kwao

Mimi nina mume ambaye tumekuwa pamoja kwa miaka minne. Ana mke wa kwanza. Huyu mwanamume anawajua watu wote wa familia yetu lakini nikimwambia twende kwao inakuwa maneno. Hivi kweli ananipenda ama ananipotezea muda?

Dada, mume wa mtu siku zote utasumbuana naye, na pia sijakuelewa vyema unaposema mke wa kwanza, ina maana umeolewa mke wa pili? Ama ndio unatumika bila takrima?

Nitakosea kulipiza kisasi?

Kuna msichana ambaye nilimuoa na baadaye tutakosana, akanisingizia maneno nikashtakiwa mahakamani na nikafungwa jela kwa miezi sita. Sasa nimetoka ninajisikia kulipiza kisasi kwa aliyonitendea. Nitakuwa nakosea nikimwadhibu huyu msichana kwa haya aliyonitendea? Naitwa Safari.

Halafu ukishalipiza kisasi unadhani utajihisi vyema? Ushauri wangu kwako ni kwamba samehe na usonge na maisha yako. Yaliyopita, yameshapita, angalia yaliyo mbele yako ambayo huenda ni mazuri kuliko hayo yaliyopita awali.

You can share this post!

HUKU USWAHILINI: Kwetu kuna wajuba magwiji wa kuwageuza...

Raila hatarini kusalia pweke katika upinzani

T L