• Nairobi
  • Last Updated February 29th, 2024 6:55 PM
UJAUZITO NA UZAZI: Kukabiliana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua

UJAUZITO NA UZAZI: Kukabiliana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua

NA PAULINE ONGAJI

WANAWAKE hufa kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua.

Mengi hutokea wakati wa ujauzito na yanaweza ‘epukika na kutibiwa. Kuna baadhi ambayo hukuwepo hata kabla ya ujauzito, lakini huzorota kiwa hayatadhibitiwa.

Matatizo mengi ambayo huwakilisha takriban asilimia 75 ya vifo vyote vya aina hii ni kuvuja damu nyingi, maambukizi na shinikizo la damu (pre-eclampsia na eclampsia). Mengine husababishwa au huhusishwa na maambukizi kama vile malaria, maradhi ya moyo au kisukari.

Lakini mbali na haya, hatari hii hutokana na kutopata huduma zinazofaa wakati wa ujauzito. Wanawake maskini wamo katika hatari kubwa ya kukosa huduma za afya wakati wa ujauzito.

Masuala hususan yanayozuia wanawake kupokea huduma wakati wa ujauzito na kujifungua ni umaskini, mwendo mrefu kufikia vituo vya afya, kutojua na kiwango duni au ukosefu wa huduma bora za afya.

Kama mwanamke mjamzito, utapunguza hatari ya kukumbwa na matatizo wakati wa ujauzito na kujijfungua kwa kuhakikisha kwamba unaanza kupokea huduma za kiafya tokea mwanzo wa ujauzito.

Hii inamaanisha kufuata ratiba ya kliniki kikamilifu na kuhakikisha kwamba unamjulisha daktari au mhudumu wa afya pindi unaposhuku kwamba kuna tatizo.

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Wali mwekundu na maharagwe ya maziwa

Mistari ya Raila yakosa kumnasa Aisha Jumwa

T L