• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 12:33 PM
MAPISHI KIKWETU: Wali mwekundu na maharagwe ya maziwa

MAPISHI KIKWETU: Wali mwekundu na maharagwe ya maziwa

NA PAULINE ONGAJI

IKIWA huna nyama usiwe na shaka.

Viungo unavyohitaji

• Mchele, vikombe -2

• Maharagwe yaliyochemshwa vikombe – 3

• Mafuta vijiko vya meza -6

• Vitunguu vlivyokatwa vipande vidogo kikombe- 3 1?2

• Kitunguu saumu kilichopondwa vijiko vya meza- 3

• Bizari kijiko cha chai -1?4

• Nyanya zilizokunwa vikombe – 5

• Mchuzi wa nyama au kuku vikombe – 2

• Maziwa vikombe – 2

• Pilipili tamu bila tembe, kata vipande vidogo -1

• Chumvi na pilipili kwa ladha

• Maji ya kutosha

Jinsi ya kutayarisha

Tia mafuta katika sufuria na uweke kwenye jiko la kiwango cha kati cha moto.

Ongeza vitunguu, kitunguu saumu, bizari na jira, kisha uvikaange huku ukikoroga kwa utaratibu kwa dakika chache hadi vitunguu vinyooke na mafuta yakolee. Ongeza nyanya na chumvi. Punguza kiasi cha moto.

Koroga kwa utaratibu hadi nyanya ziive na kuwa nyororo. Tia mchele kisha ufunike na uache utokote kwa dakika 10. Ongeza mchuzi wa nyama au kuku kisha ukoroge kwa utaratibu.

Punguza kiasi cha moto. Funika kati ya dakika 10- 15 au hadi wali uive na kuwa mkavu.

Kwenye sufuria tofauti tia vijiko 3 vya mafuta kisha uongeze maharagwe.

Kaanga maharagwe hadi yaonekane kukauka. Ongeza vitunguu na uendelee kukaanga kwa muda hadi vibadili na kuwa rangi ya hudhurungi hafifu. Tia nyanya na kitunguu saumu, koroga kwa muda, funika kwa dakika 3 au hadi mchanganyiko uwe mzito na kuwa rangi nyekundu.

Tia maji na uache maharagwe yaendelee kutokota hadi yaonekane kukauka. Ongeza maziwa kisha ufunike na upunguze kiwango cha moto hadi cha chini. Nyunyuza chumvi na pilipili, funika kwa dakika 5 zaidi.

Kwenye sinia andaa wali pamoja na maharagwe vyote vikiwa moto.

You can share this post!

BAHARI YA MAPENZI: Haki ya kumiliki mali kati ya wanandoa

UJAUZITO NA UZAZI: Kukabiliana na matatizo wakati wa...

T L