• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Minyoo wanaohangaisha watoto

UJAUZITO NA UZAZI: Minyoo wanaohangaisha watoto

NA PAULINE ONGAJI

MARADHI ya ascariasis ni mojawapo ya magonjwa hatari zaidi hasa miongoni mwa watoto kutokana na sababu huwa ni ngumu kutambua na hivyo yana uwezo wa kuharibu mwili.

Maradhi haya husababishwa na aina fulani ya minyoo inayofahamika kama Ascaris Lumbrocides.

Kadhalika utafiti unaonyesha kuwa kuna watu ambao mfumo wao wa kijinetiki unawaongezea uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.

Watu wengi na hasa watoto hugua baada ya kula chakula kilichoambukizwa na mayai ya minyoo hawa.

Baada ya mayai hayo kuangua, minyoo hujizika kwenye matumbo na baadaye kupanda kwenye mfumo wa kupumua. Baada ya haya humezwa tena na kujipanda kwenye utumbo kabla ya kuota na hata kufikia sentimeta 30.

Hatari ni kuwa ni ngumu kutambuliwa hasa wakiwa wadogo.

Ishara zake

Japo dalili za hali hii hazijitokezi kwa urahisi, hizi ni baadhi ya ishara za maradhi haya: Kuendesha, homa na tumbo kuvimba.

Wakati huu ni rahisi kwa mgonjwa kukumbwa na utapia mlo kutokana na sababu kuwa minyoo hawa huvamia virutubisho muhimu mwilini.

Ni kutokana na sababu hii ndipo unashauriwa kupata ushauri wa kimatibabu kila mara ili kujua jinsi ya kuzuia hali hii.

Jinsi ya kuzuia

•Usimpe mwanao chakula kichafu. Hii inamaanisha kwamba sharti uchunguze chakula kilikotoka ili ujue ikiwa ni safi.

•Usimpe mwanao chakula kilichoanguka chini kwani haujui kiwango cha uchafu uliojificha katika sehemu hii.

•Dumisha usafi kwa kunawa mikono na pia kumsafisha mwanao kwa sabuni kabla ya kula.•Hakikisha uchafu wa mwili na hasa choo kinatupwa mahali panapofaa.

•Kuwa na mazoea ya kumpeleka mwanao hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kila mara na kutumia dawa kuambatana na maelezo ya daktari.

 

  • Tags

You can share this post!

Mwigizaji ashtakiwa kwa kushindwa kulipa bili ya Sh152,550

TAHARIRI: Heri ahadi chache zitimiazo, kuliko rundo la hewa

T L