• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:26 PM
UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la ‘colic’ kwa mtoto mchanga

UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la ‘colic’ kwa mtoto mchanga

NA PAULINE ONGAJI

TATIZO la mtoto mchanga kuumwa na tumbo siku chache baada ya kuzaliwa au kwa Kiingereza, colic, hukumba baadhi ya watoto kati ya wiki mbili na sita baada ya kuzaliwa na kudumu kwa miezi mitatu.

Watoto walioathirika hulia na kuvuta mikono na miguu na kuonekana kana kwamba wanakumbwa na uchungu. Kunao wakati ambapo mtoto atanyosha miguu na mikono kama ishara ya uchungu huku akilia kwa nguvu.

Hali hii kwa mara nyingi hudumu kwa masaa tatu kwa siku na hutokea wakati wowote.Mtoto anayekumbwa na hali hii hulia kila wakati huku akimeza hewa na hivyo kufanya tumbo kujaa hewa na hivyo kumfanya kukosa starehe.Haimaanishi kuwa mtoto anayekumbwa na hali hii ana matatizo ya kiafya kwani ni jambo la kawaida.

Mambo ya kukumbuka kuhusu colic

Mzazi hapaswi kuhisi kana kwamba ni makosa yake Hali hii huisha mtoto anapotimu miezi mitatu Kama mzazi haupaswi kuwa na wasiswasi kwani hali hii haimaanishi kuwa mtoto wako ni mgonjwa kwani baada ya muda hali ya kawaida itarejea.

Waweza fanya nini kumtuliza mtoto

Weka chupa iliyo na maji yaliyopashwa moto kidogo kwenye tumbo la mtoto (hakikisha sio moto) Osha mtoto kwa maji yaliyopashwa moto kidogo Kwa utaratibu kanda tumbo la mtoto Mfunike mtoto kwa blanketi lenye joto Jaribu kumlisha mwanao kila baada ya masaa mawili huku ukitumia chupa lenye chuchu ndogo. Usimlishe mwanao kwa haraka Beba mwanao kwenye mapaja na umkande tumbo lake au umbebe akiwa amesimama ili kuondoa gesi kwenye tumbo.

Je napaswa kutafuta ushauri wa kimatibabu wakati upi?

Mtoto anapoonekana kukumbwa na uchungu zaidi Mtoto anapokosa kuongeza uzani Anapokumbwa na homa Unapokumbwa na wasiwasi kuwa huenda ukamuumiza mwanao.

  • Tags

You can share this post!

KIGODA CHA PWANI: Kaunti za Pwani zaweza kujikimu bila...

PENZI LA KIJANJA: Eti anataka umzalie kabla akuoe? Toroka!

T L