• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
JUMA NAMLOLA: Ababu angefanyia haya rais mwengine, angekuwa amekanyaga fremu

JUMA NAMLOLA: Ababu angefanyia haya rais mwengine, angekuwa amekanyaga fremu

Na JUMA NAMLOLA

HADITHI ya joka ndani ya kisima na msamaria mwema inajulikana na wengi waliokulia mashambani na kusimuliwa na nyanya au babu zao.

Hata vitabuni, ipo hadithi hiyo ambapo joka hilo lilipotolewa kwenye kisima, lilimgeukia msamaria na kudai tangu litumbukie kisimani halikuwa limekula, na chakula pekee kilichokuwa karibu ni huyo aliyeliokoa.

Wapita-njia waliokuta mzozo huo waliposikia kisa hicho, walitaka kujua joka hilo na ukubwa wake lilikuwa limetoshea vipi ndani ya kisima. Liliporudi kisimani kuonyesha jinsi lilivyotumbukia, yule msamaria mwema akashauriwa aokoe maisha yake.

Hapa Kenya katika muktadha wa siasa, methali akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki haina maana yoyote. Waziri Msaidizi katika wizara ya Mambo ya Kigeni, Ababu Namwamba ameonyesha jambo ambalo linadhihirisha uvumilivu wa Rais Uhuru Kenyatta.

Bw Namwamba ambaye Wakenya wamezoea kuona akiposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa anajiburudisha katika maeneo mengi ya kifahari duniani, ameamua kuwa hatajiuzulu kuwa CAS, lakini ataiponda serikali akiwa ndani.

Inawezekana amejifunza hayo kutoka kwa Naibu Rais, Dkt William Ruto. Asichofahamu Bw Namwamba ni kwamba kuku na mwewe wote wana mbawa. Lakini kuku hawezi kupaa angani.

Dkt Ruto alichaguliwa na Wakenya kwenye uchaguzi mkuu. Yeye Ababu aliteuliwa na Rais, wakati wakiwepo mamilioni ya Wakenya walio na sifa bora kumshinda.

Anapaswa kumshukuru sana Rais Kenyatta kuwa mvumilivu, anayeacha muasi kuendelea kupokea mshahara na marupurupu ya Mkenya, akiwa hajajiuzulu wadhifa wake.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Chuki: Vigogo wawadhibiti wafuasi wao

CHARLES WASONGA: Ruto na Raila wakanye wandani wao kuchochea

T L