• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 12:03 PM
KEN OKANIWA: Miaka 60 ya ushirikiano wa Kenya na Japan imekuwa na manufaa kwetu sote

KEN OKANIWA: Miaka 60 ya ushirikiano wa Kenya na Japan imekuwa na manufaa kwetu sote

NA KEN OKANIWA

MOJAWAPO ya matukio muhimu kwa mwanadiplomasia ni nchi yake inapoadhimisha kumbukumbu muhimu katika uhusiano wa taifa lake na kule aliko.

Ni furaha kwangu kuwa naiwakilisha Japan inapoadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Japani.

Matokeo ya ushirikiano huo yanaonekana katika maeneo mbalimbali. Hiyo ni pamoja na Bandari ya Mombasa, Eneo Maalumu la Kiuchumi la Dongo Kundu, Mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Ngong, ujenzi wa Vituo vya Umeme wa Jotoardhi vya Olkaria na Mpango wa Umwagiliaji wa Mwea.

Miradi hii imechangia pakubwa kuimarisha maendeleo, kiwango cha maisha, na nafasi za ajira kwa Wakenya. Japani pia imehusika na uanzishaji na kujenga uwezo wa taasisi muhimu kama vile JKUAT, KEMRI na KEFRI.

Tangu mwaka wa 1964, Japani imetuma Wajitoleaji 1,757 wa Ushirikiano wa Nchi za Nje wa Japani wanaoishi na kufanya kazi miongoni mwa jamii za Kenya. Pia imepokea wataalam 15,061 wa Kenya kwa mafunzo nchini Japani (JICA).

Maadhimisho ya miaka 60 ni tukio la kufanya upya hisia changamfu ya urafiki kati ya wananchi wa Kenya na Japani. Mkutano wa sita wa “Tokyo International Conference on African Development” (TICAD 6) mwaka wa 2016 ulikuwa hatua ya kihistoria, kwani ilikuwa ni mara ya kwanza mkutano huo ulifanyika nje ya Japani jijini Nairobi.

Katika TICAD 8 Agosti 2022, Waziri Mkuu KISHIDA Fumio alisisitiza dhamira ya Japani ya kuendelea kama “rafiki anayekua pamoja na Afrika”, ikiwa ni pamoja na Kenya, na kuahidi dola za Marekani bilioni 30 katika ufadhili wa umma na binafsi katika miaka mitatu ijayo.

Sina shaka kuzingatia umuhimu wa uhusiano kati ya nchi zetu mbili, ushirikiano na urafiki wetu utaendelea kushamiri katika miaka ijayo.

Mwandishi ni Balozi wa Japan hapa Kenya

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Kuongeza ada ya maji kutakwamisha maendeleo

Waisraeli sasa kupewa bunduki ili wajilinde

T L