• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
JUMA NAMLOLA: Natamani nipewe kazi ya uwaziri ninyoroshe wavunjao sheria za trafiki

JUMA NAMLOLA: Natamani nipewe kazi ya uwaziri ninyoroshe wavunjao sheria za trafiki

Na JUMA NAMLOLA

NDOTO ambayo imekuwa ikinijia kila ninapofunga macho usiku ni kuwa waziri katika serikali ijayo.

Sina uhakika kama hii ni kati ya zile ndoto ambazo kwetu mashambani watu huota wanapokula muhogo mchungu au la. Ninachojua ni kuwa, kama siku moja nitabahatika kupewa kazi ya uwaziri, basi nitataka nisimamie wizara ya Uchukuzi.

Marehemu John Michuki alituthibitishia kuwa inawezekana kuleta mageuzi katika sekta hiyo. Inawezekana hii haina uhusiano na ile ya Azimio la Umoja. Natumai msomaji unaona kicheko changu cha mzaha.

Naam, inawezekana kabisa kubadili mtazamo wa wakenya kuhusu usalama barabarani. Achilia mbali ajali za mabasi, matatu na magari mengine. Kutokana na sera zetu duni au utekelezaji wake, kila mwaka ni lazima Mamlaka ya Usalama na Uchukuzi (NTSA) itutangazie kuwa maelfu walikufa, hasa umapoingia msumu huu wa Krismasi.

Lakini nautamani uwaziri wa Uchukuzi ili nirejeshe nidhamu barabarani. Mara kwa mara huwa nachemka kwa hasira ninapoendesha gari kwenye barabara za jiji la Nairobi. Waendeshaji pikipiki wanaoendesha upande usiostahili, wanaovuka barabara wakiwa wanachat kwa WhatsApp, wanaosimamisha gari kwa mikono na kadhalika. Lakini wanaoniudhi zaidi, ni wanaoona gari likija na wako upande mmoja wa barabara. Watu hao hujiingiza barabarani na kujaribu kuvuka kabla gari halijawafikia.

Nani aliwaambia Wakenya kwamba wakati huu ambapo polisi wa trafiki wamekatwa mishahara, kila gari lililo barabarani lina breki imara?

Ni kwa nini wizara ya Uchukuzi isishirikiane na ile ya Elimu kubadili mtaala kuhusu sheria za barabarani? Hata rangi nyekundu, chungwa na kijani kibichi siku hizi hazina maana.

Madereva ambao haifahamiki walifuzu vipi udereva, huamua kuendesha kwenye taa nyekundu. Hali ni kadhalika kwa watembea kwa miguu na waendeshaji pikipiki. Kinachoudhi ni kuwa, lau dereva aliye makini atamgusa aliyevuka barabara kwa njia isiyofaa, umati utamzingira na pengine hata kuchoma gari lake.

Hizi ni kanuni za wapi? Kwani Kenya tumegeuka msitu wa hayawani ambapo kila mtu yuko huru kufanya apendvyo?

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Mafuriko: Mikakati ya kuzuia hasara ibuniwe

TAHARIRI: Wakenya wawe na mazoea ya kupima maradhi

T L