• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:55 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Mbona mifuko ya plastiki inaendelea kutumika?

TUSIJE TUKASAHAU: Mbona mifuko ya plastiki inaendelea kutumika?

SERIKALI, kupitia Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA), ilipiga marufuku utengenezaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki mnamo Februari 2017.

Marufuku hayo, ambayo yalilenga kuweka mazingira salama kwa binadamu na wanyama, yalianza kutekelezwa mnamo Agosti 28 mwaka huo.

Lakini miaka mitano baadaye, mifuko ya plastiki ingali imetapakaa katika miji na maeneo ya mashambani, ishara kwamba NEMA na Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) zimesahau wajibu wao wa kufanikisha utekelezaji wa marufuku hayo.

Sehemu kubwa ya mirundo ya taka katika maeneo ya mijini na mashambani ni karatasi za plastiki, ishara kwamba karatasi hizi zilizopigwa marufuku zingali zinauzwa na kutumika.

NEMA na NPS ambazo ni asasi za serikali zinafaa kutambua kwamba kwa mujibu wa kipengele cha 42 cha Katiba ya sasa kila mtu ana haki ya kuishi katika mazingira safi na salama.

You can share this post!

KCPE: Baadhi ya shule zalalama kuhusu matokeo

Kaunti yaanza matayarisho ya Madaraka Dei

T L