• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:12 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Numerical Machining Complex isiwe tu ya kutengewa bajeti bila kufanya chochote

TUSIJE TUKASAHAU: Numerical Machining Complex isiwe tu ya kutengewa bajeti bila kufanya chochote

MWEZI Mei serikali ilitangaza kuwa itapiga marufuku uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka ng’ambo kama sehemu ya mipango yake ya kupunguza ajali za barabarani.

Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa Nchini (Kebs), lilisema kuwa marufuku hayo yataanza kutekelezwa mnamo Julai 1, 2022.

“Kebs ingependa kuwaarifu wadau wote na umma kwa ujumla kwamba kuanzia Julai 1, 2022, aina mbalimbali za mabasi ya kubeba abiria na malori yaliyonunuliwa kutoka ng’ambo hayataruhusiwa kuingizwa nchini kwa ajili ya kutumika katika shughuli za uchukuzi wa mizigo na abiria,” Kebs ikasema kwenye taarifa iliyotuma kwa vyombo vya habari mnamo Mei 2, 2022.

Hizi ni habari njema kwa kampuni zinazounda magari nchini, ambazo nyingi yazo zinamilikiwa na mashirika ya kimataifa.

Lakini serikali isije ikasahau kampuni ya utengenezaji magari, Numerical Machining Complex (NMC) iliyoanzishwa wakati wa utawala wa Rais wa zamani, Hayati Daniel Arap Moi imedumaa licha ya kutengewa fedha kutoka bajeti ya kitaifa kila mwaka.

NMC ilichukua nafasi ya Shirika la Nyayo Motor Corporation iliyoanzishwa 1986 na ikaunda gari la kwanza kwa jina “Nyayo Pioneer Car 1”.

  • Tags

You can share this post!

Mbwa kusaidia kusaka mihadarati

Washirika Azimio kumnyima Raila usingizi akipita

T L