• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:54 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Ripoti yasema kaunti zote 47 zinadaiwa jumla ya Sh105 bilioni

TUSIJE TUKASAHAU: Ripoti yasema kaunti zote 47 zinadaiwa jumla ya Sh105 bilioni

RIPOTI ya hivi punde iliyotayarishwa na afisi ya Msimamizi wa Bajeti (CoB), Dkt Margaret Nyakang’o, inasema kuwa kaunti zote 47 zinadaiwa jumla ya Sh105 bilioni na wanakandarasi na wafanyabiashara huku ikisalia miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu.

Kulingana na ripoti hiyo, magavana 11 kati ya 21 ambao wanahudumu muhula wa pili na wa mwisho, ni miongoni mwa wale ambao wanadaiwa kiasi kikubwa cha fedha na wanakandarasi.

Kwa mfano, kaunti za Narok, Mombasa, Embu, Murang’a na Embu ni miongoni mwa kaunti zinazozongwa na malimbikizi ya madeni ya karibu Sh2 bilioni, kila moja.

Lakini tusije tukasahau kuwa tangu Juni 2019, Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akizitaka asasi zote za serikali kuu na zile za kaunti kulipa madeni yote yaliyothibitishwa kuwa halali.

Isitoshe, akisoma bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021-2022 bungeni mnamo Juni 10, Waziri wa Fedha Ukur Yatani ilitoa makataa ya hadi mwisho wa mwezi huo kwa magavana kulipa malimbikizi ya madeni.

Alitisha kutotoa mgao wa fedha kwa kaunti zitakazofeli kulipa madeni yao lakini inaonekana magavana wamepuuzilia mbali tishio hilo.

You can share this post!

Familia kortini kupinga hatua ya kuwahamisha

Natembeya ajitosa rasmi kusaka ugavana Trans Nzoia

T L