• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 8:50 AM
WANDERI KAMAU: Naam, Ruto anafanya vyema kuzima miungano ya kimaeneo bungeni

WANDERI KAMAU: Naam, Ruto anafanya vyema kuzima miungano ya kimaeneo bungeni

NA WANDERI KAMAU

HATUA ya Rais William Ruto kupiga marufuku miungano na makundi ya kimaeneo miongoni mwa wabunge ni mwelekeo ambao utazima chuki na mashindano ya kimaeneo ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika Bunge la Kitaifa.

Ijapokuwa hatua hiyo inafasiriwa kama pigo la kisiasa kwa baadhi ya wanasiasa kama vile Naibu Rais Rigathi Gachagua, ni nzuri kwani Bunge kwani linafaa kudumisha sifa na taswira yake kama taasisi ya kitaifa.

Katika tawala za marais Mzee Jomo Kenyatta (1963-1978) na Daniel arap Moi (1978-2002), Bunge lilikuwepo kwa jina tu.

Hata hivyo, lilikuwa limegeuzwa kuwa jukwaa la kuendeleza maslahi ya maeneo na wanasiasa fulani nchini.

Kwa mfano, Mzee Kenyatta alitumia ushawishi wake kama rais kupitisha sheria zilizoifaa familia yake, washirika na rafiki zake wa kisiasa.

Baadhi ya sheria zilizopitishwa zilihusu mashamba —hali inayotajwa kuchangia baadhi ya familia za wanasiasa maarufu nchini kumiliki mashamba makubwa makubwa katika sehemu tofauti nchini hadi sasa.

Sheria hizo ndizo pia zinalaumiwa kuchangia tatizo la uskwota katika baadhi ya maeneo, kama vile Pwani, licha ya eneo hilo kuwa na maeneo makubwa yanayoweza kutumiwa kuwatafutia makazi maskwota hao.

Katika utawala wa Moi, hali ilikuwa hivyo hivyo.

Serikali ilikuwa ikitumia ushawishi wake kuhakikisha washirika wa karibu wa Moi wameibuka washindi kwenye chaguzi kuu.

Hivyo, kwa kurejelea historia hiyo fupi, ni wazi kuwa kila mmoja anafaa kuunga mkono hatua ya Rais Ruto kuzima makundi ya wabunge ya kikanda bungeni.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Vijana wafundishwe vya bwerere havitoshi kitu

MALENGA WA WIKI: Nyakundi ni mshairi na mhariri wa riwaya,...

T L