• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 9:50 AM
20 kuwania taji la Guru Nanak Rally msimu ukifika kilele

20 kuwania taji la Guru Nanak Rally msimu ukifika kilele

Na GEOFFREY ANENE

Madereva 20 wamethibitisha kushiriki duru ya mwisho ya Mbio za Magari za Kitaifa nchini (KNRC) mwaka 2021 ya KCB Guru Nanak itakayoandaliwa katika eneo la Il-Bissel kaunti ya Kajiado mnamo Desemba 12-13.

Carl “Flash” Tundo na Baldev “Boldy” Chager, ambao wanafukuzana katika nafasi mbili za kwanza mtawalia, wanatarajiwa kuonyeshana ubabe katika mbio hizo za kilomita 154. Bingwa mtetezi wa Guru Nanak Rally Tundo ana alama 166, naye bingwa mtetezi wa kitaifa Chager 141.

Mfalme mpya wa Afrika, Tundo alishinda Equator Rally, Machakos Rally na Thika Rally, kuwa nambari mbili Ramisi Rally na nambari tatu kwa madereva wa Kenya kwenye Safari Rally na pia Voi Rally. Chager alitawala Nakuru Rally na Ramisi Rally na kukamata nafasi ya pili wakati wa Voi Rally na Thika Rally.

Onkar Rai alikuwa Mkenya wa kwanza katika Safari Rally katika nafasi ya saba mwezi Juni, Karan Patel akanyakua taji la Voi Rally naye Aakif Virani akatunukiwa ushindi wa Nanyuki Rally baada ya Tundo, Chager na Jasmeet Chana waliokuwa wafagia nafasi tatu za kwanza kupokonywa alama zote kwa kuvunja sheria za mashindano wakati duru hiyo ya saba mwezi Oktoba.

Dereva mwanamke pekee kwenye KNRC, Maxine Wahome atakuwa akiwania kutwaa taji la kitengo cha 2WD dhidi ya bingwa wa zamani Daren Miranda. Maxine, ambaye anashiriki mbio za magari kwa mwaka wake wa kwanza kabisa na pia kushirikiana na mwanadada Linet Ayuko, amekaa juu ya jedwali la daraja hiyo ya pili kwa alama 137. Daren ni nambari mbili kwa pointi 123.

Orodha ya washiriki:

Aakif Virani/Azhar Bhatti (Skoda Fabia RC2-R5) Arrow Rally

Karan Patel/Tauseef Khan (Ford Fiesta RC2-R5) Filmico Racing

Amaanraj Rai/Gurdeep Panesar (Skoda Fabia RC2-R5) Rai Racing

Carl Tundo/Tim Jessop (Mitsubishi Evolution 10 RC2-R4) Top Fry

Baldev Chager/Ravi Soni (Volkswagen Polo RC2-R5) Kabras Sugar Racing

Jasmeet Chana/Ravi Chana (Mitsubishi Evolution 10 RC2-NR4) Jaguar Petroleum

Eric Bengi/Peter Mutuma (Mitsubishi Evolution 10 RC2-NR4) Menengai Cream Racing

Piero Canobbio/Shameer Yusuf (Mitsubishi Evolution 10 RC2-R4) Kilifi Complex

Hamza Anwar/Adnan Din (Mitsubishi Evolution 10 RC2-NR4) FIA/WRC Rally Program

Nikhil Sachania/Deep Patel (Mitsubishi Evolution 10 RC2-NR4) Filmico Racing

John Ng’a ng’a/Edward Ndukui (Subaru Impreza RC2-NR4) Jungle Racing

Maxine Wahome/Linet Ayuko (Subaru Impreza RC2-NR4) Maxine Rally

Evans Kavisi/Victor Okundi (Mitsubishi Evolution 10 RC2-NR4) Evans Kavisi Racing

Ghalib Hajee/Riyaz Ismail (Mitsubishi Evolution 10 RC2-R4) Weldex

Kush Patel/Mudasar Chaudry (Subaru Impreza NAT-S) Filmico Racing

Daren Miranda/Amman Shah (Subaru Impreza RC2-NR4) Team GOA

Edward Maina/Anthony Gichohi (Subaru Impreza NAT-S) Emka Racing

Rajveer Thethy/Wayne Fernandes (Subaru Impreza RC2-NR4) R&S Racing

Sameer Nanji/Azhar Hamid (Golf MK2 NAT-2WD) Impala Motorsport

Leo Varese/Kigondu Kareithi (Toyota Auris NAT-2WD) SportPesa

You can share this post!

Junet amkataa Wanjigi

KEFWA kuandalia nyota kutoka Ligi Kuu ya wanawake tuzo ya...

T L