• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 1:47 PM
Arsenal wafika mwisho wa lami

Arsenal wafika mwisho wa lami

NA MASHIRIKA

MANCHESTER CITY wameibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza EPL 22/23 baada ya Arsenal kupoteza mchuano wao wa kufa na kupona dhidi ya Nottingham Forest waliopata bao kupitia raia wa Nigeria Taiwo Awoniyi mnamo Jumamosi ugani City Ground.

Bao la Awoniyi katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza limedumu hadi dakika ya mwisho.

Juhudi za Arsenal kutafuta bao la kusawazisha zimegonga mwamba kwani kipa wa Forest, Kaylor Navas amefanya kazi ya ziada.

Manchester City sasa ndio mabingwa huku wakiwa wanasalia na mechi tatu msimu kukamilika. Wamecheza mechi 35 na wana pointi 85 huku Arsenal waliocheza mechi 37 sasa wakifuatwa kwa pointi 81.

City kesho Jumapili watacheza dhidi ya wageni Chelsea ugani Etihad halafu Jumatano, Mei 24 watakuwa wageni wa Brighton kabla ya kukamilisha msimu dhidi ya Brentford.

  • Tags

You can share this post!

Madhehebu: Kamati teule kupendekeza Bunge libuni sheria...

Migogoro ya kisiasa kati ya magavana na manaibu wao yaenea

T L