• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Barcelona na Man-United nguvu sawa katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa Europa League ugani Camp Nou

Barcelona na Man-United nguvu sawa katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa Europa League ugani Camp Nou

Na MASHIRIKA

KOCHA Erik ten Hag alikuwa mwingi wa sifa kwa kikosi chake cha Manchester United kilichohimili presha kutoka kwa Barcelona na hatimaye kuambulia sare ya 2-2 katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa Europa League mnamo Alhamisi usiku ugani Camp Nou.

Barcelona walishuka dimbani wakipigiwa upatu wa kushinda ikizingatiwa kwamba waliwahi kuangusha Man-United mara mbili katika fainali mbili za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Chini ya kocha Xavi Hernandez, Barcelona waliwekwa kifua mbele na beki Marcos Alonso baada ya kushirikiana vilivyo na Raphinha katika dakika ya 50. Hata hivyo, Man-United walisawazishiwa na Marcus Rashford dakika mbili baadaye na wakawekwa uongozini na Jules Kounde aliyejifunga baada ya kubabatizwa na fataki ya Rashford ambaye sasa ana mabao 22 kwenye mashindano yote msimu huu.

Hata hivyo, Man-United walishindwa kudhibiti vilivyo makali ya wavamizi wa Barcelona waliofungiwa bao la pili na Raphinha ambaye ni fowadi wa zamani wa Leeds United.

Barcelona nusura wafunge bao la ushindi mwishoni mwa kipindi cha pili kupitia kwa Carlos Casemiro aliyeshuhudia mpira aliojaribu kuondoa katika eneo la hatari ukigonga mwamba wa goli la kipa wao tegemeo David de Gea.

Man-United wanaofukuzia jumla ya mataji manne muhula huu, watakuwa wenyeji wa Barcelona katika marudiano yatakayopigiwa ugani Old Trafford mnamo Februari 23, 2023.

Mshindi baada ya mikondo miwili atafuzu kuingia raundi ya 16-bora ya Europa League msimu huu wa 2022-23. Hatua hiyo ya muondoano inahusisha klabu nane zilizoambulia nafasi ya pili kwenye makundi ya Europa League, ikiwemo Man-United, ambazo zitakachuana na vikosi vilivyokamilisha kampeni ya makundi ya UEFA katika nambari ya tatu.

Man-United waliambulia nafasi ya pili nyuma ya Real Sociedad katika Kundi E la Europa League huku Barcelona wakiridhika na nafasi ya tatu nyuma ya Inter Milan na Bayern Munich katika Kundi C la UEFA.

Mara ya mwisho walipozuru uga wa Camp Nou, Man-United walipokezwa kichapo cha 3-0 chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer mnamo 2019.

Baada ya kurudiana na Barcelona, Man-United watamenyana na Newcastle United kwenye fainali ya Carabao Cup mnamo Februari 26, 2023 na huenda pambano hilo likawavunia taji la kwanza tangu wanyakue ufalme wa Europa League mnamo 2017.

MATOKEO YA EUROPA LEAGUE (Alhamisi):

Barcelona 2-2 Man-United

Ajax 0-0 Union Berlin

RB Salzburg 1-0 AS Roma

Shakhtar Donetsk 2-1 Rennes

Leverkusen 2-3 Monaco

Juventus 1-1 Nantes

Sevilla 3-0 PSV Eindhoven

Sporting 1-1 Midtjylland

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Trans Nzoia Falcons wanyorosha Kangemi Ladies kiboko kimoja...

Nani huyu anakanyaga bibi kichwani, Wakenya wataka kujua

T L