• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 8:55 AM
Beki wa zamani wa Man-United kutegemewa na Gambia kwenye AFCON 2022

Beki wa zamani wa Man-United kutegemewa na Gambia kwenye AFCON 2022

Na MASHIRIKA

CHIPUKIZI wa zamani wa Manchester United, Saidy Janko amejumuishwa katika kikosi cha Gambia kwa ajili ya fainali zijazo za Kombe la Afrika (AFCON) 2022 nchini Cameroon.

Kocha raia wa Ubelgiji, Tom Saintfiet aliongoza kikosi hicho kinachoshikilia nafasi ya 151 kimataifa kwa mujibu wa viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kushiriki fainali za AFCON kwa mara ya kwanza katika historia.

Janko ambaye ni beki wa kupanda na kushuka, kwa sasa anachezea kikosi cha Real Valladolid nchini Uhispania na atashirikiana na Ebou Adams (Forest Green Rovers) na Ibou Touray (Salford City).

Beki Omar Colley wa Sampdoria, kiungo Ebrima Darboe wa AS Roma na fowadi wa FC Zurich, Assan Ceesay ni miongoni mwa wanasoka 28 watakaotegemewa na Gambia kwenye fainali hizo za AFCON.

Pa Modou Jagne atakuwa nahodha wa Gambia nchini Cameroon. Kikosi hicho kimepangwa katika Kundi F pamoja na Tunisia, Mali na Mauritania.

KIKOSI CHA GAMBIA KWA AJILI YA AFCON 2022:

Makipa: Baboucarr Gaye (Rot-Weiss Koblenz, Ujerumani), Sheikh Sibi (Virtus Verona, Italia), Modou Jobe (Black Leopards, Afrika Kusini).

Mabeki: Pa Modou Jagne (FC Dietikon, Uswisi), Omar Colley (Sampdoria, Italia), James Gomez (AC Horsens, Denmark), Noah Sonko Sundberg (Ostersund, Uswidi), Bubacarr Sanneh (Hana klabu), Ibou Touray (Salford City, Uingereza), Saidy Janko (Real Valladolid, Uhispania), Mohammed Mbye (Solvesborg, Uswidi).

Viungo: Ebrima Sohna (Fortune FC, The Gambia), Dawda Ngum (Bronshoj, Denmark), Sulayman Marreh (Gent, Ubelgiji), Ebrima Darboe (Roma, Italy), Yusupha Bobb (Piacenza, Italia), Ebou Adams (Forest Green Rovers, Uingereza), Musa Barrow (Bologna, Italy), Ablie Jallow (Seraing, Ubelgiji), Steve Trawally (Ajman, UAE), Ebrima Colley (Spezia, Italia).

Mafowadi: Lamin Jallow (Fehervar, Hungary), Bubacarr Jobe (Norrby, Uswidi), Assan Ceesay (FC Zurich, Uswisi), Muhammed Badamosi (Kortrijk, Ubelgiji), Modou Barrow (Jeonbuk Hyundai Motors, Korea Kusini), Dembo Darboe (Shakhtyor Soligorsk, Belarus), Yusupha Njie (Boavista, Ureno).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Gumo: Alikuwa akikohoa wapinzani wanachemua

Mauritania wampanga chipukizi wa umri wa miaka 16 kwenye...

T L