• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
BIDCO imepania kumaliza nafasi ya kumi bora-FKF-PL

BIDCO imepania kumaliza nafasi ya kumi bora-FKF-PL

Na JOHN KIMWERE

BIDCO United inalenga kupambana mwanzo mwisho kuhakikisha inaibuka kati ya nafasi kumi bora kwenye Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-PL).

Kocha wa Bidco United, Anthony Akhulia yenye makazi yake katika kaunti ndogo ya Thika anasema hawana lingine bali lazima wajikaze kiume. ”Ninaamini wachezaji wangu wanatosha mboga kukaza buti na kutimiza azma yetu.

Tunalenga kurejelea mtindo wa kushinda mechi zetu,” kocha huyo alisema na kukiri kuwa tayari ubingwa wa msimu huu umewakwepa. Wikendi Bidco United ilizabwa mabao 2-1 na Kariobangi Sharks baada ya kushiriki mechi nne bila kushindwa.

Mabao hayo yalifungwa na Eric Mmata. Akizungumzia mchezo huo alisema asiyekubali kushindwa sio mshindani ambapo kupoteza ni kawaida. Aidha alisema kuwa walikuwa na nafasi nzuri kutoka nguvu sawa lakini walishindwa kusawazisha na wapinzani wao waliwapa adhabu.

Katika jedwali la kipute hicho, AFC Leopards inakamata nafasi ya kumi kwa kuzoa alama 31. Nao Maafande wa Kenya Police wameshikilia nafasi ya 11 kwa alama 28, sawa na Sofapaka FC pia Bidco United tofauti ikiwa idadi ya mabao.

Nayo Kakamega Homeboyz ingali kileleni kwa kusajili alama 52, kumi mbele ya Tusker FC baada ya kupiga mechi 24 kila moja. Katika ratiba ya kinyang’anyiro hicho, Bidco United itakutanishwa na Posta Rangers inayofunga tano bora.

You can share this post!

Gogo Boys imepania kumaliza kati ya tano bora

Baraza Kuu la ODM sasa laingilia kati mzozo kuhusu mchujo...

T L