• Nairobi
  • Last Updated June 1st, 2023 12:23 AM
CR7 achoka United, ataka kwenda zake

CR7 achoka United, ataka kwenda zake

NA MASHIRIKA

MANCHESTER, Uingereza

MSHAMBULIZI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo huenda akabanduka uwanjani Old Trafford katika kipindi hiki kirefu cha uhamisho.

Inaaminika kuwa ajenti wake Jorge Mendes anashughulikia pendekezo la kuona gunge huyo mwenye umri wa miaka 37 anarejea Juventus.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alirejea United kabla ya msimu 2021-2022 kuanza, huku viongozi wa klabu hiyo wakitumai ataisaidia kushinda angaa taji. Hata hivyo, Ronaldo alipitia ugumu chini ya makocha Ole Gunnar Solskjaer na Ralf Rangnick timu hiyo ikiambulia pakavu.

Huku Ronaldo akiwa makini kupigania mataji, inasemekana anaweza kuondoka United baada ya kuwa nayo kwa mwaka mmoja. Inasemekana kuwa Ronaldo maarufu kama CR7 pia hajapendezwa na ukimya wa United sokoni. United ya kocha Erik ten Hag imehusishwa na wachezaji Jurrien Timber, Christian Eriksen, Antony, Darwin Nunez, Frenkie de Jong na Lisandro Martinez, lakini bado haijasaini yeyote.

Aidha, United inaaminika kuongoza orodha ya timu zinazotamani huduma za Eriksen.

Klabu nyingine zinazomezea mate Eriksen ni Tottenham Hotspur, West Ham, Everton, Leicester City, Ajax na Newcastle na Brentford aliyoichezea msimu uliopita.

Inasemekana Ten Hag yuko makini kuimarisha safu ya kati baada ya viungo Paul Pogba, Nemanja Matic na Juan Mata kuhama Old Trafford mwisho wa msimu uliopita.

  • Tags

You can share this post!

Yego kuwinda tiketi ya dunia Omanyala akiahidi kutimka...

Madaktari wanane kushtakiwa kwa kifo cha Maradona

T L