• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Griezmann afikisha mabao 100 akivalia jezi za Atletico Madrid

Griezmann afikisha mabao 100 akivalia jezi za Atletico Madrid

Na MASHIRIKA

ANTOINE Griezmann alifunga bao lake la 100 kambini mwa Atletico Madrid na kuongoza miamba hao kupepeta Athletic Bilbao 1-0 katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) mnamo Jumamosi.

Goli la nyota huyo raia wa Ufaransa lilichangiwa na krosi ya Alvaro Morata aliyeshirikiana naye vilivyo katika dakika ya 47. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Griezmann kufungia Atletico tangu arejee kambini mwa kikosi hicho kutoka Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2021-22.

Matokeo hayo yalipaisha Atletico hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali la La Liga kwa alama 19, mbili pekee mbele ya Bilbao wanaofunga orodha ya nne-bora.

Bilbao walishuhudia teknolojia ya VAR ikibatilisha maamuzi ya awali ya refa kuwapa penalti kwa kudhania kuwa Reinildo Mandava alikuwa amenawa mpira ndani ya kijisanduku katika dakika ya 80.

Atletico walishuhudia jumla ya wanasoka wao sita wakionyeshwa kadi za manjano. Ushindi dhidi ya Bilbao ulikuwa wa sita kwa Atletico ya kocha Diego Simeone kushinda ligini muhula huu.

MATOKEO YA LA LIGA (Jumamosi):

Bilbao 0-1 Atletico Madrid

Girona 1-1 Cadiz

Valencia 2-2 Elche

Mallorca 0-1 Sevilla

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA WIKI, Toleo Nambari 07, Oktoba 16, 2022

MIKIMBIO YA SIASA: Gumzo mtaani MaDVD kupewa afisi...

T L