• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Gusii Starlets na Vikers Queens watamba Kombe la FKF

Gusii Starlets na Vikers Queens watamba Kombe la FKF

NA AREGE RUTH

GUSII Starlets walijikatia tiketi ya kuingia kwenye raundi ya 32 ya kombe la Shirikisho la Soka nchini (FKF), baada ya kuwalemea Migori Educational Center 2-1 ugani Kericho Green mnamo Jumapili.

Gusii ambao wanashiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Divisheni ya Kwanza (KWPLDV1) nchini, walipata bao la kwanza kupitia mshambuliaji Lydia Mogare dakika ya 28.

Elizabeth Mochoge aliongezea bao la pili dakika ya 41. Naye mchezaji wa Migori Precious DziDzie akatitiga nyavu katika dakika ya 47.

Katika uwanja uo huo, Uriri Starlets na Oserian Ladies hawakujitokeza kucheza na waliondolewa mashindanoni.

Ugani Bomet, Bomet Starlets walishindwa kuonyesha ubabe wao nyumbani baada ya kulimwa 3-0 na Vikers Queens.

Mchezaji Joan Chebet aliwapa wageni zawadi kwa kujifunga bao dakika ya 13. Mshambuliaji wa Vikers Catherine Aringo alifunga mabao mawili dakika ya 79 na 90.

Siku ya Jumamosi, Moving The Goal Post (MTG), Fortune Ladies, Kahawa Starlets na MC Millan pia walifuzu raundi ya 32 ya kombe hilo.

Zikiwa zimesalia mechi tano mkondo wa kwanza Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) kukamilika, ligi hiyo ilichukua mapumziko ya wiki moja na itarejea wikendi hii.

Matokeo mengine:

Ocean D Ladies 0-6 MTG United

Coast Starlets 2-4 Kahawa Queens

Fortune Ladies 2-0 Mukuru Talent

Patriots Queens 0-6 MC Millan Queens

Kakuma Kalobeyei 0-2 UOE

Young Bullets 2-0 Egerton

Kapsabet Starlets 2-0 MKU

Migori Educational Centre 1-2 Gusii Starlets

Bomet Starlets 0-3 Viker Queens  

  • Tags

You can share this post!

Wanafunzi wa Sekondari ya Msingi pia wapatiwe basari,...

Mwanafunzi asuka makuti akisaka karo kuingia shule ya upili

T L