• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 3:09 PM
Haaland asaidia Norway kuzamisha chombo cha Uswidi katika Nations League

Haaland asaidia Norway kuzamisha chombo cha Uswidi katika Nations League

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Erling Haaland aliendeleza makali yake katika soka ya kimataifa kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 uliosajiliwa na timu yake ya taifa ya Norway dhidi ya Uswidi katika Kundi B4 la Uefa Nations League mnamo Jumapili.

Haaland atakayechezea Manchester City msimu ujao baada ya kuagana na Borussia Dortmund, alifungulia Norway ukurasa wa mabao katika dakika ya 10 kabla ya kufunga penalti mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Nyota huyo wa zamani wa RB Salzburg sasa anajivunia mabao 20 kutokana na mechi 21 na amesalia na mabao 14 pekee kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya soka ya wanaume nchini Norway.

Haaland, 21, alichangia pia bao la tatu ambalo Norway walifungiwa na Alexander Sorloth. Bao hilo lilipachikwa wavuni baada ya Emil Forsberg kushirikiana na fowadi Dejan Kulusevski wa Tottenham Hotspur kufungia Uswidi bao la kwanza.

Viktor Gyokeres alipachika wavuni bao la pili la Uswidi dakika tano kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Tatizo la digrii lawakosesha Samboja na Sakaja usingizi

WANTO WARUI: Wamiliki shule za kibinafsi wadai kuhangaishwa...

T L