• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Tatizo la digrii lawakosesha Samboja na Sakaja usingizi

Tatizo la digrii lawakosesha Samboja na Sakaja usingizi

NA RICHARD MUNGUTI

MAPEPO ya digrii yameendelea kuwaandama Gavana Granton Samboja na Seneta wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja.

Gavana Samboja na Sakaja wanadaiwa kutohitimu kuwania ugavana kwa kuwa ‘hawana digrii’.

Wengine ambao uteuzi wao umetikiswa ni pamoja na Polycap Igathe (Nairobi), Dkt Julius Malombe (mwaniaji wa ugavana Kitui kwa tikiti ya Wiper), Timothy Olongo na Alex Musalia.

Uidhinishwaji wa Igathe umepingwa na mwaniaji George Bush anayeomba uamuzi huo wa IEBC ubatilishwe kwa madai mwaniaji huyo wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya alijiuzulu katika kazi ya unaibu wa gavana Nairobi mnamo 2017.

“Ninaomba uidhinishaji wa Igathe ufutwe kwa kuwa aliacha kazi ya unaibu gavana bila sababu,” Bw Bush anaeleza katika kesi aliyowasilisha.

Lakini Bush alijipata pabaya alipoulizwa makosa aliyofanya msimamizi wa uchaguzi katika Kaunti ya Nairobi kwa kuidhinisha uteuzi wa Igathe kuwania ugavana wakati wa uchaguzi mkuu Agosti 9, 2022.

Kizugumkuti kinachomkabili Sakaja ikiwa alihitimu kwa shahada ya digrii pia kinamkumba mwaniaji wa kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Safina Jimmy Wanjigi.

Wawaniaji wanane wa kiti cha urais ambao ari yao ilizimwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Bw Wafula Chebukati waliwasilisha malalamishi mbele ya majopo matatu yaliyozinduliwa Jumamosi.

Akiyazindua majopo hayo, Bw Chebukati alisema tayari malalamishi 262 yamewasilishwa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Wawaniaji wa kiti cha urais waliotemwa na Bw Chebukati ni Mabw Wanjigi, Reuben Kigame, Ekuru Aukot na Walter Mong’are (Nyambane) kati ya wengine.

Wawaniaji useneta watatu; Felix Aditi Awour, Bernard Makau na Zachary Momanyi waliwasilisha malalamishi mbele ya majopo matatu yaliyoanza vikao vya kutatua mizozo hiyo katika Mahakama kuu ya Milimani, Nairobi.

Akizundua majopo hayo yaliyo na wanachama tisa wakiongozwa na wakili Wambua Kilonzo, Bw Chebukati aliyataka majopo hayo yakamilishe kesi hizo katika muda wa siku 10.

“Maamuzi katika kesi hizi yatakuwa yanatolewa katika muda wa saa 48,” Bw Chebukati alisema.

Na wakati huo huo, Bw Kilonzo alisema kesi za walalamishi ambao hawatafika kortini zitatupiliwa mbali.

Afisa anayesimamia uchaguzi katika Kaunti ya Nairobi hakufika kortini Jumamosi lakini Bw Kilonzo aliamuru afike kortini Jumapili kujibu mashtaka.

Majopo hayo yalianza kufanya kazi mara moja baada ya kuzinduliwa na Bw Chebukati.

  • Tags

You can share this post!

JUNGU KUU: Wawaniaji wa ODM Nyanza hawapumui

Haaland asaidia Norway kuzamisha chombo cha Uswidi katika...

T L