• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 7:05 PM
Inter wakung’uta Juventus na kuweka hai matumaini ya kuhifadhi taji la Serie A

Inter wakung’uta Juventus na kuweka hai matumaini ya kuhifadhi taji la Serie A

Na MASHIRIKA

INTER Milan waliweka hai matumaini ya kuhifadhi ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) msimu huu baada ya kutandika Juventus 1-0 mnamo Jumapili usiku.

Inter kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu jedwalini kwa alama 63, tatu nyuma ya viongozi AC Milan na Napoli waliokomoa Atalanta 3-1. AC Milan watakuwa wenyeji wa Bologna mnamo Aprili 4, 2022.

Bao la pekee na la ushindi kwa upande wa Inter lilipachikwa wavuni na Hakn Calhanoglu aliyeshuhudia kombora lake la kwanza likipanguliwa na kipa Wojciech Szczesny. Calhanoglu alilazimika kupiga upya penalti hiyo baada ya teknolojia ya VAR kubainisha kuwa beki Matthijs de Ligt wa Juventus alihitalifiana na kuchanjwa kwa penalti ya kwanza.

Penalti yenyewe ilitokana na tukio la Alex Sandro kumchezea visivyo Denzel Dumfries mwishoni kwa kipindi cha kwanza.

Ushindi wa Inter ulikuwa wa kwanza kutokana na mechi saba zilizopita huku Juventus wakipigwa kwa mara ya kwanza ligini tangu Novemba 2021.

AS Roma ya kocha Jose Mourinho inakamata nafasi ya tano kwa alama 54 baada ya kulaza Sampdoria 1-0 ugenini. Bao hilo la Roma lilijazwa kimiani na kiungo wa zamani wa Arsenal na Man-United, Henrikh Mkhitaryan.

MATOKEO YA SERIE A (Aprili 3, 2022):

Juventus 0-1 Inter Milan

Fiorentina 1-0 Empoli

Atalanta 1-3 Napoli

Udinese 5-1 Cagliari

Sampdoria 0-1 Roma

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mbappe ang’aa PSG ikiponda Lorient ligini

MUME KIGONGO: Kiasi kidogo cha pombe japo hatari, huboresha...

T L