• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 4:43 PM
MUME KIGONGO: Kiasi kidogo cha pombe japo hatari, huboresha mbegu za kiume – Utafiti

MUME KIGONGO: Kiasi kidogo cha pombe japo hatari, huboresha mbegu za kiume – Utafiti

NA LEONARD ONYANGO

WANAUME wamejipata katika njiapanda kuhusu ubugiaji wa pombe huku watafiti wakidai kuwa kiasi kidogo kinaweza kusaidia kuboresha mbegu za kiume.

Utafiti uliofanywa nchini Italia na hospitali ya Granda Ospedale Maggiore Policlinico, ulibaini kuwa kiasi kidogo cha pombe kinasaidia kuongeza kiasi cha mbegu za kiume.

Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanaume 323 ulibaini kuwa watu waliokuwa wakinywa angalau chupa moja ya bia kwa wiki, walikuwa na kiasi kikubwa cha mbegu za kiume ikilinganishwa na wenzao ambao hawatumii kileo au wanaobugia pombe nyingi kupindukia.

Tafiti nyingine pia zimedai kuwa kiasi kidogo cha pombe kinasaidia afya ya moyo.

Lakini tafiti mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni zimehusisha pombe na maradhi hatari kama vile kansa, shinikizo la damu, kisukari na hata matatizo ya moyo – hata ukinywa kiasi kidogo.

Utafiti uliochapishwa wiki iliyopita katika jarida la JAMA Network Open umekosoa ripoti ya utafiti wa hospitali ya Policlinico ukisema kuwa pombe kidogo ni hatari kwa afya.

Utafiti huo uliofanywa nchini Amerika miongoni mwa watu 371,463 unasema kuwa kuna uwezekano kwamba watu wanaokunywa kiasi kidogo cha pombe kwa wiki pia wanapata lishe bora kama vile kula matunda, mbegu, nafaka na mboga.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka jana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Oxford ulihusisha kiasi kidogo cha pombe na dosari katika ubongo.

You can share this post!

Inter wakung’uta Juventus na kuweka hai matumaini ya...

Gogo Boys imepania kumaliza kati ya tano bora

T L