• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Isuzu yazindua gari la kipekee ‘Eliud Kipchoge 1:59 Isuzu D-Max’

Isuzu yazindua gari la kipekee ‘Eliud Kipchoge 1:59 Isuzu D-Max’

Na AYUMBA AYODI

MAGARI maalum ya “Eliud Kipchoge 1:59 Isuzu D-Max Limited” yamezinduliwa kwa heshima ya bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Isuzu East Africa Rita Kavashe na mshikilizi wa rekodi ya marathon ya wanaume duniani Kipchoge walizindua gari hilo la rangi ya chungwa katika kiwanda cha kutengeneza magari kinachopatikana kwenye barabara ya Mombasa Road.

Meneja Mkuu wa Mauzo wa Isuzu East Africa Kevin Ochieng pia alihudhuria hafla hiyo.

Ochieng alisema kuwa magari hayo machache yatakuwa na alama ya 1:59 kusherehekea mafanikio ya ushirikiano na Kipchoge atakayepata fursa ya kwanza kuendesha gari hilo la kwanza maalum 001.

Kipchoge anashikilia rekodi rasmi ya dunia ya mbio za kilomita 42 baada ya kutawala Berlin Marathon 2022 kwa saa 2:01:09.

Yeye pia ni binadamu wa kwanza kumaliza umbali huo chini ya saa mbili. Alikamilisha mbio maalum za INEOS1:59 kwa saa 1:59:41 mjini Vienna, Austria mnamo Oktoba 12, 2019. Eliud Kipchoge 1:59 Isuzu D-Max inatokana na ufanisi wa INEOS1:59.

“Tutakuwa na magari 159 kwa hivyo wanaoyataka wafanye hima,” alisema Ochieng’.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Serikali yakana madai kuwa wadukuzi wa Kichina waliingilia...

Mswada wa Fedha wa 2023 kuchangia kupanda kwa bei ya unga...

T L