• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 7:05 PM
Jinsi Man-City walivyopoteza nafasi ya kurejea kileleni mwa jedwali la EPL

Jinsi Man-City walivyopoteza nafasi ya kurejea kileleni mwa jedwali la EPL

Na MASHIRIKA

BEKI Kyle Walker amesema matokeo ya kikosi chao cha Manchester City “hayakubaliki” baada ya sare ya 1-1 waliyolazimishiwa na Nottingham Forest kuwanyima nafasi ya kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Bao la Chris Wood mwishoni mwa kipindi cha pili lilifuta juhudi za Bernardo Silva aliyewaweka Man-City uongozini katika dakika ya 41.

“Tumepoteza alama mbili muhimu hapa. Tulipata nafasi nyingi za wazi za kufunga Forest. Inatulazimu kujitahidi na kuanza kusajili matokeo bora. Hatuna sababu ya kutofanya hivyo ikizingatiwa idadi kubwa ya wachezaji wa haiba kambini mwetu,” akasema Walker.

Erling Haaland alishuhudia fataki yake ikigonga mwamba wa lango baada ya kombora la Aymeric Laporte kuokolewa na kipa wa Forest, Keylor Navas.

Bao la Wood aliyefunga kwa mara ya kwanza ndani ya jezi za Forest lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Morgan Gibbs-White.

“Simlaumu yeyote. Iwapo wavamizi hawapati bahati ya kufunga, basi ilikuwa kazi ya mabeki kubana kabisa safu yao ya ulinzi na kuhakikisha kwamba tunatia kapuni alama zote tatu,” akaongeza Walker.

Matokeo hayo dhidi ya Man-City yaliendeza msururu wa matokeo bora ya Forest ambao sasa hawajashindwa katika mechi nane mfululizo. Man-City kwa upande wao waliteremka hadi nafasi ya pili na hivyo kupitwa na Arsenal waliokomoa Aston Villa 4-2 ugani Villa Park.

“Tulijitahidi sana Jumatano iliyopita kuwatandika Arsenal. Ingawa alama tatu tulizojizolea wakati huo hazijapotea, ipo haja kwa kikosi kuwa thabiti na kushinda takriban kila mchuano iwapo kina ndoto ya kuhifadhi ufalme wa EPL muhula huu,” akaongezea difenda huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.

Man-City sasa wamepoteza alama 15 katika mechi zao za ugenini kwenye EPL msimu huu. Miamba hao walidondosha pointi 11 pekee ugenini msimu wa 2021-22 na kujizolea ubingwa wa EPL kwa pointi 93, moja pekee mbele ya Liverpool walioambulia nafasi ya pili.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Liverpool yafufuka

Msimamizi wa kanisa achomoa kitambulisho cha askari jela...

T L