• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Kenya kuvaana na Nepal mechi 8 za kriketi Nairobi

Kenya kuvaana na Nepal mechi 8 za kriketi Nairobi

Na GEOFFREY ANENE

WANAKRIKETI wa Kenya wako tayari kukaribisha Nepal kwa mechi tano za Twenty20 na tatu za ODI zitakazosakatwa Agosti 25 hadi Septemba 5 katika klabu ya Nairobi Gymkhana, Nairobi.

Katika viwango bora vya kimataifa vya Twenty20, Kenya ni nambari 30 nayo Nepal inakamata nafasi ya 14 kwa hivyo hazitakuwa mechi rahisi kwa wenyeji. Nepal pia ni taifa lililo na hadhi ya ODI ambayo Kenya iliwahi kuwa nayo kati ya 1996 na 2014 kabla ya kupoteza kwa sababu ya matokeo yasiyoridhisha katika mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2015.

Hapo Agosti 23, mratibu wa mashindano yatakayokutanisha Kenya na Nepal, Walter Trenk alisema kuwa maandalizi yamekamilika.

Itakuwa mara ya kwanza Kenya ni mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya kriketi baada ya muda mrefu.

Trenk alisema kuwa wapenzi wa kriketi hawatalipia chochote kutazama mechi. Pia, alihakikishia mashabiki usalama wao. Nepal ya kocha Manoj Prabhakar iliondoka Bara Asia Jumatatu na inatarajiwa mapema leo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Kriketi Kenya, Manoj Patel anaamini kuwa mchezo wa Kenya utaimarika kupitia ushirikiano na Nepal. Waziri wa Michezo Amina Mohamed amealikwa siku ya kufungwa kwa mashindano hayo. Timu ya Kenya inatiwa makali na David Obuya.

Kikosi cha Kenya:

Alex Obanda, Sukdeep Sigh, Irfan Karim, Rakep Patel, Collins Obuya, Sachin Budhia, Nelson Odhiambo, Emmanuel Bundi, Eugene Ochieng, Vraj Patel, Elijah Otieno, Shem Ngoche (nahodha), Lucal Oluoch na Nehemiah Odhiambo.

  • Tags

You can share this post!

Shirika kupeleka maji mitaa duni

Atalanta yapiga AC Milan breki kali ligini

T L