• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Kipa Ederson Moraes sasa kudakia Man-City hadi 2026

Kipa Ederson Moraes sasa kudakia Man-City hadi 2026

Na MASHIRIKA

KIPA Ederson Moraes wa Manchester City amerefusha muda wa kuhudumu kwake ugani Etihad kwa miaka miwili zaidi hadi 2016.

Kipa huyo raia wa Brazil alisajiliwa na Man-City mnamo 2017 na amesaidia miamba hao kutia kapuni mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Kufikia sasa, amewajibikia mabingwa hao watetezi wa EPL jumla ya mechi 194.

Ederson ndiye mwanasoka wa tano wa haiba kubwa kambini mwa Man-City kusajili mkataba mpya mwaka huu wa 2021 baada ya Kevin de Bruyne, Fernandinho, John Stones na Ruben Dias.

“Maamuzi ya kutia saini mkataba mpya yalikuwa mepesi. Hakuna popote pengine ambapo ninatamani kuwa. Kuwa sehemu ya kikosi hiki ni azimio la kila mwanasoka. Nia kuu kwa sasa ni kuendeleza kujituma na kutwaa mataji mengi iwezekanavyo. Man-City wana jukwaa zuri zaidi la kufanya hivyo,” akasema mlinda-lango huyo.

Tangu aingie katika sajili rasmi ya Man-City kutoka Benfica miaka minne iliyopita, Ederson amenyanyua Kombe la FA, mataji manne ya League Cup na matatu ya EPL.

Katika jumla ya mechi 194 ambazo amechezea Man-City, kipa huyo mwenye umri wa miaka 95 amepiga jumla ya mechi 95 bila ya kufungwa bao na ametawazwa Kipa Bora wa EPL kwa misimu miwili.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Rais Conde alivyochotwa na makomando wa kijeshi

IEBC yakana ‘kumsaidia’ Ruto