• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 AM
Lengo la Murang’a Seal ni kusaidia vijana kutimiza ndoto yao ya kusakata soka ya kulipwa

Lengo la Murang’a Seal ni kusaidia vijana kutimiza ndoto yao ya kusakata soka ya kulipwa

NA JOHN ASHIHUNDU

KUSHIRIKI katika Ligi Kuu ya Kenya sio nia kuu ya klabu ya Murang’a Seal, bali ni kunoa vipaji vya vijana na kuhakikisha wanasajiliwa na klabu za soka ya kulipwa hapa nchini na kule ng’ambo ili wapate kujikimu kimaisha.

Mapenzi yake ya soka yalimfanya Wakili Robert Macharia kuanzisha klabu hii kwa lengo la kutafuta chipukizi wenye vipaji na kuwasaidia kunoa vipawa vyao, kabla ya kujiunga na klabu mbalimbali.

“Nilianzisha klabu hii kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye talanta kutoka sehemu hii ili wapate fursa ya kusakata soka ya kulipwa kokote watakapoitwa kuendeleza vipaji vyao ili watimize ndoto yao ya kusakata soka ya kulipwa,” alisema Macharia.

Murang’a Seal kwa sasa ingekuwa inashiriki katika ligi kuu ya Kenya kama sio mchanganyiko uliotokea baada ya Shirikisho la Soka Nchini (FKF) kupiga marufuku matokeo ya msimu uliopita wa 2021/2022.

Klabu hii ilicheza mechi mbili za mchujo dhidi ya Wazito FC, lakini licha ya kushindwa kutokana na idadi ya mabao, Wazito ilikuwa imetangaza kujiondoa ligini, hivyo nafasi hiyo ineachiwa Murang’a Seal.

Uongozi wa soka ulikuwa chini ya kamati ya mpito, lakini Serikali ya Kenya Kwanza ilipotwaa usukani, iliamua kurejesha FKF ambayo iliharamisha matokeo ya msimu uliopita, hivyo kuzima ndoto za Murang’a Seal.

Murang’a Seal (Sports Excellence Academy Limited) itapigana kuwa kituoa bora zaidi cha kunoa vipaji vya vijana nchini na eneo zima la Afrika Mashariki kwa lengo la kuuza vijana katika klabu maarufu barani Ulaya.

“Ni kweli, kucheza ligini kunawapa wachezaji fursa ya kuonyesha vipaji vyao hadharani, lakini lengo leti ni kugundua vipawa mapema ili wasaidiwe kuimarisha vipawa vyao wangalipo wachanga, wakati wakiendelea kupata elimu ya kawaida shuleni,” alisema Robert Macharia ambaye ndiye mwenyekiti wa klabu hii.

Mweyekiti wa klabu ya Murang’a Seal Bw Robert Macharia baada ya mazoezi. PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Macharia anasema, tayari klabu hii imepata ekari 26 za ardhi ambayo itatumika kujenga uwanja wa kisasa, vyumba vya wachezaji, mkahawa, zahanati, ukumbi wa burudani, ukumbi wa mazoezi ya viungo, kidimbwi, madarasa, viwanja vya mazoezi, mbali na uwanja wenyewe wa kuchezea mechi.

“Tunataka wachezaji wapata elimu ya kawaida wanapojifunza kusakata boli kama ilivyo katika vituo vya kunoa vipaji kule ng’ambo,” aliongeza.

Alisema lengo lake ni kapata wachezaji kuanzia umri wa miaka 10 ambao wataishi kwenye kituo hicho hadi watakapofika umri wa miaka 18, wakati wakimaliza masomo yao ya Kidato cha Nne.

“Hapa, watafunzwa mbili mbali za kusakata soka wakati wakipata masomo ya kawaida hadi watimie umri wa miaka 18. Katika umri huo, baadhi yao wataendelea kucheza kandanda, wakati wengine wakijiunga na vyuo kwa masomo ya juu,” alisema Macharia.

Macharia alianza mradi huu baada ya kutembelea vituo mbali mbali jijini London alikopata fursa ya kushuhudia mechi ya Premia kati ya Arsenal na Manchester City.

“Kwa kweli nilivutiwa na miundo mbinu yao, lakini niligundua kwamba hata hapa nyumbani tuna vipaji vya hali ya juu miongoni mwa wachezaji ambao iwapo watapaililiwa vizuri, watakuwa bora kama wale wanaoonekana televisheni moja kwa moja kila wakati ,” alisema.

“Niliposhuhudia wakicheza, kwa hakika hakuna tofauti kubwa na viwango vya hapa nchini, lakini huku wanaandaliwa wangalipo wadogo, na kuonekana mapema. Kadhalika, kuna ufadhili wa kutosha pamoja na uungwaji mkono wa utawala, kuliko ilivyo hapa nchini.”

“Nilitembelea kituo cha Southampton Academy na kuvutiwa na mipango yao kwa jumla. Huko, wanaandaliwa kuanzia umri wa miaka 10 hadi 17, na ni miongoni mwa vituo vinavyotoa wachezaji wengi kwa timu nchini Uingereza.”

“Tuko na mpango, na tutasajili vijana bila ubaguzi wowote na kusaidia vijana walio na hamu ya kujifunza soka kwa maisha yao ya baadaye,” alisema

Macharia alijaribu kuungana na Serikali kuukarabati uwanja wa Mumbi Stadium, lakini hakufurahia jinsi ujenzi huo ulipokuwa ukifanyika na ikabidi aache.

“Niliamua kuunda uwanja wangu katika mradi huu uliogharimu Sh300,000. Nilitafuta nyasi bora na kufikia sasa najivunia unavyoonekana kwa sasa,” alisema.

Aliyekuwa kocha wa Sofapaka, Ezekiel Akwana ndiye aliyepewa usukani kusimamia idara ya ukufunzi, wakati akiwa kama kocha mkuu wa Murang’a Seal.

  • Tags

You can share this post!

Wafugaji wapinga New-KCC kubinafsishwa

WANDERI KAMAU: Utawala wa Ruto ujenge uwiano si ulipizaji...

T L