• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Marcelo apata hifadhi mpya nchini Ugiriki baada ya kubanduka Real Madrid

Marcelo apata hifadhi mpya nchini Ugiriki baada ya kubanduka Real Madrid

Na MASHIRIKA

BEKI mzoefu raia wa Brazil, Marcelo Vieira, ameingia katika sajili rasmi ya Olympiakos ya Ligi Kuu ya Ugiriki baada ya kuagana na Real Madrid ya Uhispania.

Marcelo, 34, ndiye mchezaji anayejivunia mataji mengi zaidi katika historia ya Real aliowaongoza kutwaa makombe 25 katika kipindi cha miaka 15.

Alijinyanyua taji lake la sita la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na la tano katika soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu jana baada ya kutandaza michuano 18 chini ya kocha Carlo Ancelotti.

Ametia saini mkataba wa mwaka mmoja kambini mwa Olympiakos watakaokuwa huru kurefusha kandarasi hiyo kwa miezi 12 zaidi kutegemea matokeo.

Marcelo aliyechezea Real mara 546, anajivunia kusakatia Brazil mara 58 tangu mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia wamwajibishe kwa mara ya kwanza mnamo 2006.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Barcelona wafaulu kumng’oa beki Marcos Alonso kambini...

Kenya yashindwa nyumbani na Nepal taji la ODI

T L