• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Marumo Gallants anayochezea Mkenya Ovella Ochieng’ yatimua kocha Migne

Marumo Gallants anayochezea Mkenya Ovella Ochieng’ yatimua kocha Migne

Na GEOFFREY ANENE

HAKUKALIKI Marumo Gallants inayoajiri Mkenya Ovella Ochieng’ baada ya klabu hiyo kutimua kocha Mfaransa Sebastien Migne mnamo Jumapili.

Klabu hiyo inashiriki Ligi Kuu ya soka nchini Afrika Kusini.

Chama cha Wachezaji wa Soka nchini Afrika Kusini (SAFPU) kilitisha kushtaki Marumo kwa kusimamisha kazi wachezaji watatu (Tholang Masegela, Aluwani Nedzamba na Simon Mamudzidi) kwa muda mapema mwezi huu kwa kile tovuti ya kickoff ilidai kuwa “waliadhibiwa kwa kuitisha malimbikizi ya mshahara wao”.

Marumo sasa imeamua kupiga kalamu Migne kwa kile imetaja “kudharau mkurugenzi wa kiufundi wa klabu hiyo Harris Choeu katika uwanja wa ndege wa OR Tambo kabla ya mechi dhidi ya Golden Arrows jijini Durban”.

Klabu hiyo, ambayo iliajiri kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya mnamo Julai 1 mwaka 2021, imesema kuwa Migne anafaa kuwa mstari wa mbele kufanya kikosi kiwe na nidhamu.

“Katika kikao cha kusikiza kesi yake kilichofanywa Oktoba 7, 2021, Migne alipatikana na kosa la kukaidi na kutumia lugha ya matusi dhidi ya mkurugenzi wa kiufundi Harris Choeu,” tovuti hiyo ilisema.

Ochieng’ hakuachiliwa na klabu hiyo ajiunge na Harambee Stars kwa mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Mali mnamo Oktoba 7 na Oktoba 10. Alinyakuliwa na Marumo mnamo Ahosti 19 kutoka Vasalunds IF inayovuta mkia kwenye Ligi Kuu ya Uswidi.

You can share this post!

Atakubali mistari ya Raila?

Waumini wafokea pasta dikteta