• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:01 AM
Mashabiki wa Shabana waweka historia kwa kujaza uwanja wa Mbaraki licha ya kukomolewa

Mashabiki wa Shabana waweka historia kwa kujaza uwanja wa Mbaraki licha ya kukomolewa

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MASHABIKI wa soka wa Shabana FC waliweka rekodi mpya ya kuujaza uwanja wa Mbaraki Sports Club wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya FKF, Jumapili, Novemba 6, 2023.

Washika dau wa soka wa Kanda ya Pwani wakiongozwa na kocha wa Bandari FC John Baraza wametoa wito kwa watu wa eneo hilo waige mfano wa Shabana wa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.

Katika mchezo huo, mashabiki wa Bandari ambao huwa wanatamba dhidi ya wapinzani wao wanaofika kucheza na timu yao, walifunikwa na wale wa Shabana ambao walikisiwa kuwa zaidi ya asilimia 75.

Baraza amsema umati wa mashabiki uliofurika katika kiwanja wengi wao walikuwa wa Shabana ambao waliwapa motisha wachezaji wao.

“Ningeliomba mashabiki wetu wa Pwani nao wawe wakijitokeza kwa wingi ili kuwapa moyo wanasoka wao wafanye vizuri katika kila mechi,” akasema Baraza.

Kwa mara ya kwanza uwanja huo umekuwa na watazamaji wengi ambao hata katika mzunguko wa watu kusimama, ulikuwa umejaa. Hata mechi zinazohusisha klabu zenye mashabiki wengi zaidi nchini Gor Mahia na AFC Leopards hazijawahi kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki kama hao.

Kuhusu mchezo huo, Baraza amesema hakuna timu rahisi kwenye ligi kuu hata zile zilizoko nafasi za chini ya ngazi za ligi hiyo zinaweza kupata ushindi zikikutana na timu kubwa.

Mkufunzi huyo alifurahia kuona katika mechi hiyo, wachezaji wake wameweza kuitumikia kona kufunga bao.

“Nilifurahikia kuona kona moja imezalisha matunda na tutaangazia zaidi ili vijana wetu wawe wakifunga mabao mengi kupitia kona,” akasema.

Naibu kocha wa Shabana FC Oscar Kambona amesema watakwenda kufanya marekebisho ya makosa waliyotekeleza na hasa kutotumia nafasi nyingi za kufunga mabao walizopata.

“Nawashukuru mashabiki wetu kwa kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu na nawaomba waendelee kufanya hivyo tukiwaahidi tutafanya bidii kuhakikisha timu inashinda kuwaridhisha wapate kufurahia,” akasema Kambona.

 

  • Tags

You can share this post!

Pokot Magharibi KCSE yaendelea vyema maeneo hatari usalama...

Bodaboda, wanachuo wapanda migomba kwenye barabara mbovu...

T L