• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 7:50 AM
Masogora tisa wanaopiga soka ya EPL waitwa kambini mwa timu ya taifa ya Brazil

Masogora tisa wanaopiga soka ya EPL waitwa kambini mwa timu ya taifa ya Brazil

Na MASHIRIKA

WANASOKA tisa wanaochezea vikosi mbalimbali vya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wameitwa na kocha Adenor ‘Tite’ Bacchi kambini mwa timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya mechi mbili zijazo za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 dhidi ya Ecuador na Paraguay.

Makipa Alisson Becker (Liverpool) na Ederson Moraes wa Manchester City ni miongoni mwa masogora hao. Wengine ni beki Thiago Silva wa Chelsea, wavamizi Gabriel Jesus (Man-City), Roberto Firmino (Liverpool), Richarlson Andrade (Everton) na viungo Douglas Luiz (Aston Villa), Fabinho (Liverpool) na Fred wa Manchester United.

Kwa mujibu wa Tite aliyemtupa nje beki Marcelo wa Real Madrid tangu fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi, maamuzi ya kumjumuisha Fred kambini mwake yamechochewa na haja ya kutaka kiungo huyo ashirikiane na difenda Renan Lodi wa Atletico Madrid ambaye sasa ni kizibo rasmi cha Marcelo.

Brazil wameshinda mechi zote nne zilizopita za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar baada ya kumwajibisha kikosini beki Luiz wa Villa.

Hata hivyo, nyota huyo atakosa mchuano ujao dhidi ya Ecuador kutokana na marufuku aliyopigwa katika mechi ya awali.

Licha ya kupigiwa upatu wa kuunga kikosi cha Brazil, fowadi Raphinha Belloli wa Leeds United bado amekosekana kwenye mipango na mawazo ya kocha Tite.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

IEBC yataka waliochochea vurugu Juja wachukuliwe hatua kali...

Theo Walcott apokezwa mkataba wa kudumu ugani St Marys kwa...