• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Mbappe aongoza PSG kuzamisha Monaco ligini

Mbappe aongoza PSG kuzamisha Monaco ligini

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe alifunga mabao mawili na kusaidia Paris Saint-Germain (PSG) kukung’uta AS Monaco 2-0 katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Jumapili.

PSG ya kocha Mauricio Pochettino iliponea chupuchupu kufungwa bao la mapema na Sofiane Diop wa Monaco aliyegonga mhimili wa lango la wenyeji wao.

Bao la Mbappe lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Djibril Sidibe na Angel di Maria ndani ya kijisanduku. Goli hilo lilikuwa la 100 kwa nyota huyo raia wa Ufaransa katika soka ya Ligue 1. Lionel Messi ndiye alichangia goli hilo la pili la PSG.

PSG walioanza kipindi cha pili kwa matao ya chini walinusurika pia kufungwa mabao kupitia Guillermo Maripan aliyeelekeza idadi kubwa zaidi ya makombora langoni.

PSG ambao ni mabingwa watetezi wa Ligue 1, sasa wametandaza jumla ya mechi tisa mfululizo bila kupigwa ligini. Ilivyo, dalili zote zinaashiria ugumu wa mshindani yeyote kuwazuia kutwaa taji la Ligue 1 ambalo Lille walilinyanyua mnamo 2020-21.

Huku PSG wakijivunia alama 45 kileleni mwa jedwali, Monaco wanakamata nafasi ya nane kwa pointi 26 sawa na nambari saba Strasbourg. Olympique Marseille wanashikilia nafasi ya pili kwa pointi 32, moja kuliko Rennes na mbili zaidi kuliko Nice wanaofunga orodha ya nne-bora.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Jumapili):

PSG 2-0 Monaco

Lille 0-0 Lyon

Angers 0-1 Clermont

Metz 4-1 Lorient

Rennes 1-2 Nice

Troyes 1-2 Bordeaux

Strasbourg 0-2 Marseille

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Barcelona washuka zaidi ligini baada ya kukabwa koo na...

Real Madrid wakomoa Atletico kwenye gozi kali la Madrid

T L