• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Modric sasa kuchezea Real Madrid hadi Juni 2024

Modric sasa kuchezea Real Madrid hadi Juni 2024

Na MASHIRIKA

LUKA Modric ametia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja utakaomshuhudia sasa akichezea Real Madrid ya Uhispania hadi Juni 2024.

Mkataba kati ya Real na kiungo huyo mzoefu raia wa Croatia ulitarajiwa kukatika rasmi mwishoni mwa Juni 2023 na akawa anahusishwa na uwezekano mkubwa wa kubanduka ugani Bernabeu na kuyoyomea Saudi Arabia kunogesha Ligi Kuu ya Pro-League.

Modric, 37, amechezea Real mara 488 huku akisaidia miamba hao kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na matano ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) tangu asajiliwe kutoka Tottenham Hotspur mnamo 2012.

Modric pia alitawazwa taji la Ballon d’Or mnamo 2018 baada ya kuongoza Croatia kutinga fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi ambapo walikutana na Ufaransa waliowapepeta 4-2.

Modric anatia saini kandarasi mpya kambini mwa Real baada ya wanasoka Toni Kroos, Dani Ceballos na Nacho Fernandez. Anatazamiwa kuwa mhimili mkubwa wa mabingwa hao mara 14 wa UEFA baada ya nyota Karim Benzema kusajiliwa na Al-Ittihad ya Saudi Arabia.

Real tayari wamesajili kiungo mvamizi raia wa Uingereza, Jude Bellingham, kutoka kwa Borussia Dortmund.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Maandalizi ya Eid-ul-Adha yashika kasi

Nation FC yapangwa katika Kundi C michuano ya SJAK

T L