• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mshindi wa Kundi C kati ya Italia na Uswisi kuamuliwa na mechi ya mwisho baada ya Jorginho kupoteza penalti

Mshindi wa Kundi C kati ya Italia na Uswisi kuamuliwa na mechi ya mwisho baada ya Jorginho kupoteza penalti

Na MASHIRIKA

JORGINHO Frello alipoteza penalti ya dakika ya mwisho katika mechi ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia mnamo 2022 dhidi ya Uswisi mnamo Ijumaa usiku.

Tukio hilo linamaanisha kwamba mshindi wa kwanza wa Kundi C kati ya Uswisi na Italia sasa ataamuliwa na mechi ya mwisho. Kufikia sasa Italia wanaselelea kileleni kwa alama 15 sawa na Uswisi walio na uchache wa mabao. Jorginho alipaisha penalti ambayo Italia walipokezwa baada ya teknolojia ya VAR kubainisha kwamba Ulisses Garcia alikuwa amempiga kumbo Domenico Berardi ndani ya kijisanduku.

Giovanni Di Lorenzo alisawazishia Italia katika dakika ya 36 baada ya Silvan Widmer kuwaweka Uswisi kifua mbele katika dakika ya 11. Chini ya kocha Roberto Mancini, Italia watakutana na Ireland Kaskazini ugenini katika mchuano wao wa mwisho kundini mnamo Novemba 15 huku Uswisi wakialika Bulgaria.

Italia ambao ni washikilizi wa taji la Euro, watapania kushinda mechi hiyo kwa matumaini kwamba Bulgaria watawabana Uswisi ili kuepuka mchujo wa mikondo miwili zaidi ya kuamua mshindi wa Kundi C. Italia waliwahi kukosa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi baada ya kuzamishwa na Uswidi kwenye michuano ya mikondo miwili ya mchujo.

Uswisi nao waliishia kushiriki mchujo wa kufuzu miaka minne iliyopita ila wakapepeta Ireland Kaskazini na kujikatia tiketi ya kunogesha fainali za 2018 nchini Urusi.

You can share this post!

Simbas mawindoni kulipiza kisasi dhidi ya Namibia raga ya...

Kane afunga mabao matatu na kuongoza Uingereza kuponda...

T L