• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
N’Golo Kante ajiondoa katika timu ya taifa ya Ufaransa itakayovaana na Ivory Coast na Afrika Kusini

N’Golo Kante ajiondoa katika timu ya taifa ya Ufaransa itakayovaana na Ivory Coast na Afrika Kusini

NA MASHIRIKA

KIUNGO matata wa Chelsea, N’Golo Kante, amejiondoa katika kikosi cha Ufaransa kwa sababu za kibinafsi.

Nyota huyo alijumuishwa katika timu ya taifa inayojiandaa kupimana nguvu na Ivory Coast pamoja na Afrika Kusini katika michuano miwili ijayo ya kirafiki.

Kante alitua kambini mwa Ufaransa mnamo Machi 21, 2022 na akashiriki kipindi kimoja cha mazoezi. Hata hivyo, kwa mujibu wa kituo cha RMC Sport, sogora huyo wa zamani wa Leicester City aliondoka “kwa sababu za kibinafsi”.

Kujiondoa kwa Kante ni pigo kubwa kwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ambaye pia atalazimika kukosa huduma za difenda tegemeo Presnel Kimpembe wa Paris Saint-Germain (PSG) kutokana na ugonjwa.

Zaidi ya nahodha na kipa Hugo Lloris ambaye pia anauguza jeraha la mguu, Deschamps atakosa maarifa ya fowadi mahiri wa Real Madrid, Karim Benzema na nyota wa Bayern Munich, Benjamin Pavard. Huku kipa Mike Maignan wa AC Milan akitarajiwa kujaza pengo la Lloris, Olivier Giroud na William Saliba pia wameitwa kambini katika dakika za mwisho kujaza mapengo yaliyoko.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wakenya waanza kuvuna medali michezo ya walemavu ya Dubai...

Amerika yaionya Urusi dhidi ya kutumia silaha za kemikali...

T L