• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 8:55 AM
Omanyala ni miongoni mwa walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya Mashujaa Dei

Omanyala ni miongoni mwa walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya Mashujaa Dei

Na SAMMY WAWERU

MSHIKILIZI wa rekodi ya Kenya mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala ni miongoni mwa walioalikwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya Mashujaa Dei 2021, leo Jumatano.

Sherehe hizo zimeandaliwa katika Kaunti ya Kirinyaga, na kufuatia janga la Covid-19 idadi ya watu 3, 000 pekee ndio wanatarajiwa kuhudhuria.

Maadhimisho hayo yanafanyika katika uwanja wa Wang’uru, na ambao una uwezo kusitiri idadi jumla ya watu 10, 000.

Mbali na viongozi wakuu serikalini, wanasiasa, wageni mashuhuri, baadhi ya wanamuziki na wanariadha waliozolea Kenya nishani mbalimbali wamewasili katika uga huo.

“Ni shime kuu kutambuliwa kama mmoja wa mashujaa wa Kenya,” akasema Bw Omanyala.

Taifa linasubiri kuona iwapo nyota huyo atakuwa kati ya watakaotuzwa na Rais Uhuru Kenyatta atakayeongoza maadhimisho hayo, kupitia tuzo za shime kwa Wakenya waliochangia kuboresha taifa, HSC Award.

Omanyala ameshiriki mashindano kadha; Riadha za Diamond League ya Brusseles, Austria na Kip Keino Classics.

You can share this post!

VYAMA VYA KISWAHILI: Chama dawa mjarabu kukabili mitazamo...

Tusker FC yawasili Misri kutafuta miujiza dhidi ya Zamalek...

T L