• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 6:44 AM
Pele: GOAT, Mfalme, hakuna anayefikia kiwango chake

Pele: GOAT, Mfalme, hakuna anayefikia kiwango chake

NA JOHN ASHIHUNDU

KIPAJI cha Edson Arantes do Nascimento maarufu Pele kiligunduliwa akiwa mtoto mdogo na kikamkweza hadi upeo wa kabumbu na kumfanya kuenziwa kama mchezaji bora zaidi kuwahi kusakata soka katika karne ya 20.

Kwa Kimombo wanamtambua kama G.O.A.T. – Greatest Of All Time!

Iwapo tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka (Ballon d’Or) ingekuwepo enzi zake, bila shaka kabati lake lingefurika ukiongeza makombe si haba aliyojishindia.

Ndiye alikuwa supastaa wa kwanza kabisa wa kabumbu kwa umaarufu aliozoa sio tu katika klabu yake ya Santos nchini Brazil lakini kote ulimwenguni.

Ni hadhi aliyokoleza kwa kuwa mwanasoka pekee duniani kushinda Kombe la Dunia mara tatu – 1958, 1962 na 1970.

Jagina huyo alianza kusakata soka akiwa chini ya umri wa miaka 10 akisakatia timu kadhaa mtaani.

Aliongoza kikosi cha Bauru Athletico kwenye mashindano matatu ya vijana ya kitaifa, na hapo ndipo kipaji chake kilipoonekana, kabla ya baadaye kocha Waldemar de Brito kumpeleka Santos FC kufanya majaribio akiwa na umri wa miaka 15.

Makocha wote waliomshuhudia kwenye majaribio hayo walikubaliana na kipaji chake cha kipekee, ambapo mwaka mmoja baadaye alijiunga na kikosi kikuu cha Santos, na kifunga bao katika mechi ya kwanza, kabla ya kuibuka mfungaji bora ligini mwaka huo.

Miezi 10 baadaye, aliitwa kujiunga na timu ya taifa ya Brazil kutokana na kiwango chake bora, licha ya umri wake mdogo.

Kwa waliomfahamu kwenye, kisoka, Pele alikuwa binadamu wa kipakee aliyekuwa mkarimu, alijali maisha yaw engine, mbali na kuwa mnyenyekevu.

Kutokana na umaarufu wake, wananchi wengoi wa taifa la Brazil wanaoishi ng’ambo walirejea nyumbani kumpa heshima zao za mwisho.

Waombolezaji walimiminika ugani Santos Stadium mapema kupiga foleni, huku wakibeba maua mikononi.

Alikuwa na wake watatu- Rosemeri dos Reis Cholbi tangu 1966 hadi 1982, Assira Nascimento (1994-2008) na Marcia Aoki 2016-2022). Watoto wake ni pamoja na Edinho, Sandra, Regina Arantes do Nasimento.

Pele aliaga dunia Desemba 29 akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua saratani ya utumbo mpana kwa muda mrefu. Lakini historia kamwe haitamsahau.

  • Tags

You can share this post!

Wazazi wapigania CDF wakidai imefaa wengi

CECIL ODONGO: Mgogoro kati ya Moi na Salat katika chama cha...

T L