• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:54 PM
Presha kwa Bayern baada ya kichapo kutoka kwa Gladbach kuwaweka katika hatari ya kupitwa

Presha kwa Bayern baada ya kichapo kutoka kwa Gladbach kuwaweka katika hatari ya kupitwa

Na MASHIRIKA

BAYERN Munich wako katika hatari ya kupitwa na nambari mbili Borussia Dortmund na namba tatu Union Berlin kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) baada ya kupokezwa kichapo cha 3-2 na Borussia Monchengladbach mnamo Jumamosi ugani Borussia Park.

Wenyeji Monchengladbach walijiweka uongozini kupitia kwa Lars Stindl katika dakika ya 13, sekunde chache baada ya beki Dayot Upamecano kuonyeshwa kadi nyekundu. Ingawa Eric Maxim Choupo-Moting alisawazishia Bayern kabla ya kipenga cha kuashiria mwanzo w kipindi cha kwanza kupulizwa, Jonas Hofmann na Marcus Thuram walirejesha Gladbach kifua mbele.

Mathys Tel alifunga bao la pili la Bayern mwishoni mwa kipindi cha pili na kufanya mambo kuwa 3-2. Japo matokeo hayo yalisaza Bayern kileleni mwa jedwali la La Liga kwa alama 43, ni pengo la ubora wa mabao pekee ndilo linatamalaki kati yao, Borussia Dortmund na Union.

Bayern, wanaofukuzia ufalme wa taji la Bundesliga mara 11 mfululizo, sasa wamepoteza mechi tano zilizopita dhidi ya Gladbach. Union Berlin walitoka sare ya 0-0 wakicheza dhidi ya Schalke 04 katika uwanja wao wa nyumbani wa An den Alten Forsterei jana Jumapili.

Borussia Dortmund, walifikia Bayern kwa alama 43 kileleni mwa jedwali kwa kuangusha wanyonge Hertha Berlin ugani Signal Iduna Park mnamo Jumapili, Februari 19, 2023. Bayern wana ubora wa mabao 40 huku Dortmund wakiwa na 17 nao Union Berlin wakiwa na ubora wa mabao 11.

MATOKEO YA BUNDESLIGA (Jumamosi):

M’gladbach 3-2 Bayern Munich

Stuttgart 3-0 Cologne

VfL Bochum 0-2 Freiburg

Wolfsburg 0-3 RB Leipzig

Frankfurt 2-0 Werder Bremen

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wanajeshi wa Ulinzi Starlets waahidi kupigana vilivyo...

Real Madrid wakomoa Osasuna na kuendelea kuifuata Barcelona...

T L