• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Wanajeshi wa Ulinzi Starlets waahidi kupigana vilivyo kutetea taji la Kombe la FKF

Wanajeshi wa Ulinzi Starlets waahidi kupigana vilivyo kutetea taji la Kombe la FKF

NA AREGE RUTH

KOCHA mkuu wa timu wanajeshi wa Ulinzi Starlets Joseph Mwanzia, ana imani kwamba timu yake ina uwezo wa kutetea taji la kombe la Shirikisho la Soka nchini (FKF) ambalo limeingia awamu ya 32.

Mabingwa hao watetezi wa kombe hili walishinda makala ya kwanza baada ya kuichapa Vihiga Queens 2-0 mnamo Jumamosi, Oktoba 2, 2021 katika Uwanja wa Maonyesho wa Nakuru (ASK).

Mashindano hayo ambayo yalianzishwa rasmi mwezi Januari mwaka 2020, hayajawahi kufanyika tangia mwaka tena baada ya kuhairishwa kutokana na mlipuko wa Virusi vya Uviko 19.

“Tunasubiri tu tupate ratiba ya jinsi tutakavyocheza. Lengo letu ni kutetea taji letu ambalo tumelihifadhi kwa miaka mitatu sasa. Kila mechi na katika kila hatua ya makundi tutachukulia kwa umuhimu sana,” amesema Mwanzia.

“Tunataka kuanza maandalizi ya mapema. Tunapo pambania taji ya ligi pia tunaendelea kujinoa kwa ajili ya shindano hilo. Ifikapo wakati huo, wachezaji wangu tegemeo watakuwa wamepona majeraha baada ya kukaa nje kwa muda mrefu,” aliongezea Mwanzia.

Vichuna Vihiga ambao ni vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), Gaspo Women na mabingwa watetezi Thika Queens ambao wanashikilia nafasi ya pili na tatu kwenye jedwali, wamejumuishwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Timu nyingine za KWPL ni pamoja na Nakuru City Queens, Bunyore Starlets, Zetech Sparks, Kisumu All Starlets, Kangemi Ladies na Kayole Starlet.

Timu za Ligi Kuu ya Wanawake za Divisheni ya Kwanza (KWPLDV1L) zikiwemo Kibera Soccer Ladies, Falling Waters Barcelona, Mombasa Olympics, Sunderland Samba, Soccer Sisters, Eldoret Falcons, Kisped Queens, Bungoma Queens, Gideon Starlets na Royal Starlets pia zimejumuishwa.

Baada ya mechi za raundi ya kwanza ambazo zilichezwa wikendi iliyopita, timu zifuatazo zilijikatia tiketi ya raundi ya 32; Moving The Goal Post (MTG), Kahawa Queens, Fortune Ladies, Macmillan Queens, Chuo Kikuu cha Eldoret (UOE), Young Bullets, Kapsabet Starlets, Gusii Starlets, Kolwa Falcons, na Vickers Queens, Coast Starlets na Migori Educational Centre.

Hatua ya 32 itachezwa Machi 18, 2023. Raundi ya 16 inatarajiwa kuanza Aprili 15, 2023. Robo fainali zitapigwa mnamo Mei 20, 2023. Mechi za nusu fainali zitafanyika Juni 24, 2023, na fainali itachezwa Julai 2, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Obiri atawala Ras Al Khaimah Half, Koech aongoza wanaume...

Presha kwa Bayern baada ya kichapo kutoka kwa Gladbach...

T L